Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali inadhamiria kuanzisha Kanzi Data ya kutambua makundi ya Damu kwa Watanzania wote, ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa Damu Salama kwa watu wenye makundi adimu ya Damu.
Kwa Mujibu wa Ripoti iliyotolewa na Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwamba inayo kanzi Data ya Watu takribani 350 ambao wapo kwenye Kundi O-Negative baada ya kuwatambua kama Kundi adimu la Damu.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo Aprili 11, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika ofisi za mpango wa Taifa wa Damu Salama ili kukagua na kuangalia hali ya upatikanaji wa damu hapa nchini.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu Akizungumza katika mkutano huo
Waziri Ummy pia amepongeza hatua ya watu takribani elfu ishirini (20,032) ambao walijitokeza kuchangia Damu katika kipindi cha wiki ya matendo ya huruma kwa waumini wa kanisa la Waadventista wa Sabato, Kampeni ya kitaifa ya robo mwaka ya tatu na sikukuu ya pasaka.
Vile vile ameipongeza timu ya Yanga kwa kufanikisha ukusanyaji wa damu takribani chupa 544 kwa siku moja
“Nitumie fursa hii kuwapongeza ambao wamekuwa na utaratibu wa kuchangia Damu mara kwa mara ikiwemo kundi lililojitokeza kuchangia damu katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka” amesema Waziri Ummy.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy amekemea tabia ya baadhi ya watumishi katika sekta ya afya kuwauzia Damu wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt Abdu Juma amemueleza Waziri Ummy baadhi ya changamoto zinazokabili mpango wa Taifa wa Damu Salama ikiwemo ile ya ukosefu wa magari ya Kukusanyia Damu pamoja na vichomea Taka.
SOMA TAARIFA HII MUHIMU HAPA
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









