Mwanamume aliyeshtakiwa kwa kumuua mke wake miaka kadhaa iliyopita nchini Uhispania sasa anadaiwa kumuua wakili wake na kisha kujitoa uhai .
Jose Javier Salvador Calvo, 50, aliruka kutoka kwenye daraja la mji wa mashariki wa Teruel polisi walipojaribu kumkamata.
Kisa hicho kimewagutusha watu nchini Uhispania na kuzua mjadala mkali kuhusu sheria ya mzozo wa kinyumbani nchini humo.
Akizungumzia vifo hivyo waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez ameapa kuendeleza juhudi za kukabiliana na visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Tunafahamu nini kufikia sasa?
Jose Javier Salvador Calvo alimpiga risasi na kumuua mke wake, Patricia Maurel Conte, 29, mwezi Mei mwaka 2003 katika eneo la Aragon kaskazini mashariki mwa Uhispani.
Baada ya kuachilia chini ya sheria maalum mwaka 2017, muuaji huyo alijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na Rebeca Santamalia Cáncer, 47,wakili aliyemtetea mahakamani aliposhtakiwa kwa mauaji,kwa kujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.
Polisi ilimpata wakili huyoakiwa ameuawa kwa kudungwa kisu katika nyumba ya Salvador Calvo iliyopo eneo la Aragon siku ya ijumaa baada ya mume wake kupiga ripoti kuwa ametoweka.
Muda mfupi kabla ya saa sita usiku mwili wa mshukiwa aliyejirusha kutoka daraja la Teruel, mji uliyopo kilo mita 150 kutoka eneo la tukio, ulipatikana na polisi waliyokuwa kazini.
Mwakilishi wa mamlaka ya mtaa huo Carmen Sánchez amewaambia wanahabari kuwa wakili huyo alikua mhasiriwa wa “unyanyasaji wa kijinsia”.
Ukatili dhidi ya wanawake ni mbaya kiasi gani Uhispania?
Katika mtandao wake wa Twitter, waziri mkuu Sánchez amesema kuwa wanawake wanne wameuawa nchini Uhispania siku za hivi karibuni na kwamba ipo haja ya kuingilia kati ”jinamizi” hilo
from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2FKnRAc
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







