Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo ameongoza watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kupanda miti zaidi ya elfu moja (1000) katika eneo la Mji wa Serikali, inapojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri Makamba amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu na takribani miti 1000 ya aina ya mdodoma inayostahimili ukame imepandwa hii leo. “Sisi ni watu wa Mazingira, ni lazima tuonyeshe mfano, hapa kila mtumishi atakuwa na wajibu wa kutunza miti atakayokabidhiwa na kuhakikisha inakua” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amesema kuwa Jiji la Dodoma linakabiliwa na changamoto ya mandhari kutokana na ardhi yake kuwa kame na kupelekea uoto wa asili kupungua kwa kiasi kikubwa. Hivyo, ametoa wito kwa kila taasisi na Idara kuunga mkono kwa vitendo kampeni iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Novemba 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani, kwa kupanda miti kwa wingi katika Mji wa Serikali na Dodoma kwa ujumla ili uwe mji wa mfano kwa kuwa na mandhari yakuvutia.
“Kwa kuwa sisi ndio wasimamizi wa Mazingira, upandaji na usimamizi wa miti ni sehemu ya Hifadhi ya Mazingira, hivyo lengo la Ofisi yetu ni kuonyesha mfano, watumishi wote kuanzia Waziri mpaka Mhudumu kila mmoja atakuwa na miti yake ya kutunza na kuhakikisha inakua” Makamba alisisitiza.
Awali Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea eneo inapojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais na kuridhishwa na kasi ya ujenzi katika eneo hilo na kumtaka Mkandarasi wa Mradi kutoka (Vikosi vya Ujenzi) Mhandisi Simeo Machibya kukamilisha kazi yote kwa wakati. “Ujenzi huu ufanyike usiku na mchana” Makamba alisisitiza.
Katika zoezi la leo Waziri Makamba ameambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo, Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali.
from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2s5vQ2W
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







