Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amefanya kikao na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi mikoa yote Tanzania Bara kutathmini siku 100 za uongozi wake tangu ameanza kuiongoza wizara hiyo.
Kikao hicho kilichofanyika Desemba 21, 2023 jijini Dodoma ambapo Mhe. Waziri Silaa amekutana Menejimenti ya Wizara, Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kujitatnmini katika kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi bora ya ardhi.
“Hiki ni kikao kazi cha kutathmini siku 100 na kutengeneza mpango wa kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi na kuwahudumia wananchi wetu” amesema Mhe. Waziri Silaa.
Waziri Silaa amewasisitiza Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kuwa wana kazi ya kusimamia watumishi walio chini yao kwa kujipanga vizuri na wana uwezo kubadilisha jinsi sekta ya ardhi inavyoendeshwa nchini kote.
Waziri Silaa ameongeza kuwa Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wanachapa kazi vizuri katika mikoa yote, utendaji kazi wao utafanya taswira ya Wizara iende mbele kutekeleza maelekezo ya viongozi wa kifaifa na kuleta tija kwa watanzania.
Aidha, Waziri Silaa amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na wataendelea kupokea na kuheshimu ushauri wanaoutoa kuhusu shughuli za sekta ya ardhi nchini.
Awali akimkaribisha Mhe. Waziri kwenye kikao hicho, Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga amesema kuwa Menejimenti ya Wizara na taasisi zilizochini ya Wizara kwa kushirikiana na Makamishna Wasaidiza wa mikoa wapo tayari kupokea maelekezo ya Mhe. Waziri kwa kuwa ndiye mwongoza njia ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi katika sekta ya Ardhi.

Mhe. Waziri Silaa ametimiza siku 100 katika nafasi hiyo ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 30, 2023 na kuapishwa Septemba 01, 2023.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









