Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo limewataka wafanyabiashara wa kuuza nyama kuhakikisha wanauza nyama ambazo zimegongwa mihuri toka mamlaka zinazohusika.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua Januari 18 mwaka huu wakati alipotembelea mabucha ya kuuza nyama katika Soko Kuu la Arusha.

ACP Pasua amewataka wauza nyama wote kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu zinazowaongoza sambamba na kuuza nyama ambazo zinatoka katika machinjio ya Serikali ambapo mifugo inapimwa kabla ya kuchinjwa.
Naye mkuu wa Soko hilo Bwana Datus Renatus mbali na kupongeza jeshi la Polisi, amesema wamejifunza mambo mengi kupitia maelekezo mbalimbali ambayo wameyapata kutoka Polisi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wa nyama kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu za biashara zao.
Mwenyekiti wa Mabucha Soko kuu la Arusha Bwana Ezekiel Michael amesema wamepokea changamoto ambazo wameambiwa na kuhaidi kuzifanyia kazi lakini pia akawataka wafanyabiasha wa nyama kucha tabia ya kununua mifugo ya wizi badala yake wanunue ile ambayo imefuafa taratibu.
Naye bwana Laban Kivuyo ambaye ni muuza nyama katika soko hilo ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea kuwa karibu nao kwani kupitia ukaribu huo taarifa nyingi za kihalifu zitaripotiwa.
Pia amewataka wafanyabiashara wanaopokea mali za wizi haswa mifugo kuacha tabia hiyo kwani Serikali ipo makini badala yake wafanye kazi zinazotambulika kisheria zitakazowaingizia kipato halali.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







