UTURUKI KUISAIDIA TANZANIA KUFANIKISHA MPANGO WA ELIMU BURE..SOMA ZAIDI HAPA

Admin Updates9 years ago7 Views


Serikali ya Uturuki imeahidi kuisaidia  Serikali ya Tanzania kufanikisha mpango wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi utakaoanza January mwakani.

Hayo yalizungumzwa jana na Balozi wa Uturuki nchini Bi Yasemin Eralp  alipokuwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu alipomtembelea ofisini kwake.

Balozi yasemin  Eralp aliainisha Serikali ya Uturuki imekuwa  ikisaidia  Tanzania katika miradi mbalimbali nakuwa na ushirikiano wa Mabunge  ya nchi hizo mbili ambao umeongeza mahusianio mazuri ya nchi hizo, mbali na ushirikiano wa Bunge ameweka wazi kuwa serikali yake ya Uturuki  inaweza kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwezesha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, ujenzi wa maktaba za shule,ujenzi wa viwanda na ujenzi wa vituo vya Afya na Hospitali nchini.

“Katika kuunga  mkono mpango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa elimu bure kwa watanzania kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari tuko tayari kushirikiana na serikali kwa kutoa msaada  wa vifaa kwa wanafunzi kama vile vitabu, kompyuta na kujenga maktaba katika shule mbalimbali”alisema Balozi Eralp.

Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu aliishukuru Serikali ya Uturuki kwa kusaidia  Tanzania katika miradi ya kimaendeleo na kuzidi kuomba ushirikiano zaidi toka kwao hasa katika maswala ya Bunge katika nchi hizo.
 
“Tunaishukuru Serikali ya Uturuki kwa ushirikiano wao  katika  maswala ya Bunge na kujenga mahusiano mazuri na Tanzania na  hata katika miradi ya maendeleo ya jamii inayofadhiliwa na serikali ya Uturuki na tunaomba tuendeleza mahusiano zaidi katika mahusiano ya mabunge ya nchi hizi mbili ” alisema Dkt Tulia.

Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Uturuki katika maswala ya Bunge na mwaka 2010 wawakilishi toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Mhe. Samwel Sitta walitembelea Bunge la Uturuki kwa mwaliko wa aliyekuwa  Spika wa Bunge la Uturuki wakati huo Mhe.  Mehmet Ali Sahim.
Mpekuzi blog
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.