Moja ya Mambo ambayo kwa tafiti mbalimbali humjenga na kumfanya mwanadamu awe bora sana ni kuweza kujizuia kuwa ni wakati gani useme,wakati gani usiseme na ni mahali gani unasemea..Leo katika safari yetu ya kujifunza kwa viongozi wetu wa Chama na Serikali tumepita katika ukurasa wa Instagram wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Ndg.Atufigwe Kasesela (Pichani) ambapo ameandika maneno mazito na ya hekima kubwa kuhusu faida ya kujifunza kunyamaza hasa kwa wenye mamlaka na hata wasio na mamlaka ambapo ameandika haya……
1. Kunyamaza wakati fulani maishani mwako siyo kipawa bali ni nidhamu
(1 Wathesalonike 4: 11).
2. Nyamaza unapohisi hasira
(Mithali 14:17).
3. Nyamaza unapokuwa huna taarifa ya kutosha au ukweli kuhusu unachotaka kusema (Mithali 18:13).
4. Nyamaza unapokuwa ni wakati wako kusikiliza na kujifunza
(Mithali 13: 1).
5. Nyamaza ukigundua kwamba maneno yako yataleta picha mbaya
(Mithali 17: 27).
6. Nyamaza ukijua kile unachotaka kusema kitaharibu jina na sifa ya mwenzio
(Mithali 16: 27).
7. Nyamaza ukijua utakachosema kitaharibu urafiki na kujeruhi mwenzako
(1Wakorintho 15: 33).
8. Nyamaza ukigundua kwamba utaaibika baadaye kwa sababu ya ulichokisema
(Mithali 8:8).
9. Nyamaza ukijua unachotaka kusema kitamdhalilisha Mungu, wewe mwenyewe au familia yako
(1Petro 2: 21-23).
10. Nyamaza ikiwa wakati ulio nao ni wakati wa kazi
(Mithali 14: 23).
11. Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, atajilinda nafsi yake na taabu
(Mithali 21: 23).
Mungu akupe neema ya kujenga nidhamu ya kunyamaza kwa maana maneno ya kinywa chako ni mtego kwako
(Mithali 6:2).
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 - Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33