
Na Ashrack Miraji
Watu 37 wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Sabasaba, kata ya Same, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.
Ajali hiyo imetokea juni 28, 2025 majira ya jioni baada ya basi la kampuni ya Channel One lenye namba za usajili T 179 CWL lililokuwa likitoka Moshi kuelekea Tanga kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Coaster lenye namba za usajili T 199 EFX lililokuwa likitoka wilayani Same. Magari yote mawili yalishika moto na kusababisha vifo hivyo vya kuhuzunisha.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, ambaye ametembelea eneo la tukio na kuwatembelea majeruhi hospitalini, amesema ajali kama hiyo haijawahi kutokea mkoani humo na kuitaja kama msiba mkubwa kwa taifa.
“Mpaka sasa Watanzania 37 wamefariki, tunao majeruhi 29 ambapo 24 wapo hapa katika Hospitali ya Mji Same na wengine watano wamekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi na KCMC. Kwa kweli ni msiba mkubwa,” amesema Mhe. Babu.
Ameongeza kuwa serikali imeanza utaratibu wa upimaji wa vinasaba (DNA) kwa miili ya marehemu ili iwe rahisi kutambua ndugu na jamaa zao kutokana na miili hiyo kuungua vibaya na kutotambulika kirahisi.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewaomba wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za ndugu zao ambao hawajawaona kuanzia leo ili kujiridhisha kwa kuwa bado kuna miili haijatambuliwa
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro amesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la basi la kampuni ya Channel One lililokuwa likitoka Moshi kuelekea Tanga na kusababisha basi hilo kupoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na Coaster, kabla ya magari yote kuwaka moto.
Taarifa zaidi kuhusiana na ajali hii zitaendelea kutolewa kadri uchunguzi na zoezi la utambuzi wa miili unavyoendelea.

Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






