Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Agosti, 2016 amemuapisha Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.Dkt. Modestus Francis Kipilimba ameapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam na mara baada ya kuapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Salome Kaganda.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Modestus Francis Kipilimba amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye amestaafu.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika Makungu kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania Bara.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Robert Msalika Makungu alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.
Wakurugenzi na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi zao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
24 Agosti, 2016




Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






