
Mkuu wa Mkoa wa ametoa agizo kwa vyombo vya usalama Mkoa wa Dodoma kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo vya kikatili vilivyoibuka hivi karibuni kwa watoto ikiwemo mauaji na kukatwa baadhi ya viungo vya mwili katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara alioufanya na wananchi wa Kata ya Ipagala kwenye ofisi za Kata hiyo Jijini Dodoma Julai 22, 2024 wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.
“Jambo la Mtoto kutekwa halivumiliki na Serikali. Matukio haya yanafahamika na yanafanyiwa kazi na yeyote atakayebainika kuhusika, atachukuliwa hatua za kisheria. Natoa agizo kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka kwa matukio yanayosababisha vifo ili jambo hili lifike mwisho” RC Senyamule.
Aidha, agizo hilo limefuatia kero iliyowasilishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa huyo na moja kati ya wakazi wa eneo hilo aliyelalamikia uwepo wa matukio hayo kwenye eneo lao sambamba na kuiomba Serikali ijenge kituo cha Polisi kwenye Kata hiyo.
Akitoa jawabu la kero hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya, amesema tayari Serikali imetangaza ujenzi wa vituo vya Polisi kwenye kila Kata japo kuwa kama jamii inauhitaji wa haraka inashauriwa kujenga kwa nguvu zao boma la kituo na Serikali itamalizia.
Mkutano huo uliibua kero mbalimbali zikiwemo ardhi na maji na zote zilipatiwa majawabu ambapo Mkurugenzi wa Jiji atafungua kliniki fupi ya ardhi Julai 24 katika eneo hilo huku DUWASA wakitarajia kutekeleza mradi wa shilingi Bilioni 10.2 utakaotatua kero ya maji safi na mradi wa uboreshaji maji taka kwa gharama ya shilingi Bilioni 164.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








