Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Albert Chalamila, amesema upungufu na kutokuboreshwa kwa Mabasi ya Mwendokasi ni vitendo vya kuwahujumu Wananchi wanaotumia usafiri huo ni hujuma dhidi ya juhudi za serikali hususan katika kuleta maendeleo na kuwahudumia Wananchi.
Akiwa Kituoni hapo asubuhi ya leo Julai 24, 2025, katika ziara kwenye Kituo cha Mwendokasi Kimara Mwisho kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu upungufu wa Mabasi hayo, Chalamila amesema hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na kuonya kuwa serikali haiwezi kuvumilia uzembe huo unaojirudia kila mara.
Chalamila amesema tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo takribani miaka Tisa iliyopita, hakuna jitihada zozote zilizochukuliwa kuboresha au kuongeza Mabasi, hali inayosababisha msongamano na kuchelewesha safari za Wananchi.

Mkuu wa Mkoa pia amehoji ni kwa namna gani mtu binafsi anaweza kutumia gari moja kwa miaka tisa mfululizo bila kufikiria kulibadilisha, achilia mbali magari ya umma yanayohudumia maelfu ya Watanzania kila siku.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameonya kuwa kama wahusika wa usimamizi wa huduma hiyo hawatabadilika na kuchukua hatua madhubuti mara moja, basi atapendekeza wachukuliwe hatua kali, ikiwemo kuondolewa kwenye nyadhifa zao.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






