PIGO CHADEMA: Timu yote iliyokuwa inamuunga mkono Mbowe yajiondoa CHADEMA rasmi, Soma zaidi hapa

Admin Updates1 month ago8 Views

 BREAKING: Timu Yote iliyokuwa Ikimuunga Mkono Mbowe Yajiondoa Chadema

“Sisi tumeamua wote kwa pamoja tunajiondoa Chadema ili tuwaachie hicho chama waendeshe wanavyotaka kwasababu sisi hatuwezi kuwa sehemu, hatuwezi kuwa wanachama wa Chama ambacho maamuzi yake hayafanywi kwa vikao, hatuwezi kuwa wanachama wa chama ambacho wanachama wanabaguliwa, hatuwezi kuwa wanachama wa chama ambacho Katiba haifuatwi. Hatuwezi kuwa wanachama wa namna hiyo kwasababu sisi sio chawa, sisi ni Viongozi, sisi tunajitambua na tuliingia Chadema kwasababu ya malengo na tunatoka Chadema kwasababu Chadema imeachana na malengo yaliyotufanya tuingie.

Kwa hiyo tunajitoa Chadema ili wasipate sababu kwamba Chama hiki kilikufa kwasababu walikuwepo. Na ili nisiwaachie maswali mtu anaweza akauliza sasa tunaenda wapi, sisi sio wazee wa kufikia umri wa kustaafu. Tutaendelea kuwapigania watanzania na tutatafuta jukwaa muafaka.”-Benson Kigaila, Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika kati ya waliokuwa Wajumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA taifa mpaka tarehe 22 Januari 2025, na wanahabari mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatano.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.