Msanii wa nyimbo za Injili, Bonny Mwaitege amesikitishwa na taarifa za watu katika mitandao ya kijamii wanaomzushia kifo.
Akizungumza nasi leo Jumatatu Julai 22, 2024 amesema kuwa yeye ni mzima wa afya na amesikitishwa na uzushi huo unaosambazwa mitandaoni.
“Aise pole sana dada yangu, mimi ni mzima wa afya njema wala sijafa. Huu uzushi tu wa watu ukweli nimesikitika sana, maana nimeanza kupigiwa simu na watu kutokea Nairobi na Dar na mikoa mingine, hii ni mbaya sana. Hapa sasa hivi nipo njiani naelekea Nairobi kwenye kazi za injili, Mungu ni Mwema,” amesema Mwaitege.
Alipoulizwa iwapo uzushi huo kuwa ametengeneza kiki, amesema sio kiki kwani kwa hatua aliyopo sio wa kutaka kufanya kitu atumie kiki.
“Kwa nini nifanye kiki? Yaani kiki ndio nijiue mwenyewe? Kwa hatua niliyofikia ya kazi ya sanaa yangu sio ya kufanya kiki ndio nifanye kitu,” amesema Mwaitege.
Mwimbaji huyo amewahi kutamba na nyimbo nyingi zikiwemo Safari Bado, Dunia Dunia, Acha Nizaliwe, Bado Nampenda, Mke Mwema, Sisi Sote, Imba, Mama na Neema Imenibeba na nyingine.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







