Mhandisi Makene Madoshi:Ni lazima tumuunge Mkono Rais Samia katika kutunza na kuhifadhi Mazingira

Admin Updates1 month ago5 Views

 

     Mhandis Dkt.Helladius Makene Madoshi
Mtaalamu mbobezi wa Masuala
na tafiti na usimamizi wa Mazingira nchini Tanzania Dkt.Mhandisi Helladius Makene
Madoshi amewataka watanzania kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha mazingira ya Nchi yetu kupitia
maelekezo mbalimbali anayoyatoa yanaendelea kutunzwa na kuwa salama na oevu
vikiwepo vyanzo vya maji
 kwa ajili ya usatwi
wa jamii na viumbe hai kwa ujumla.

Akizungumza jijini Mbeya
wakati alipokuwa na semina ya uelimishaji jamii kuhusu umuhumu wa kulinda
vyanzo vya maji na kupanda miti, katika mahojiano maalumu kuhusu nini kifanyike
ili kuhakikisha mazingira ya kila siku ya watu na viumbe hai yanakuwa salama Dr.Madoshi
amesema kwa sasa anafurahishwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kwenye
maeneo mbalimbali zinakofanyka shughuli za kijamii zenye lengo la kuhifadhi
mazingira tofauti na miaka ya nyuma ambapo eneo hilo halikuwa limetolewa elimu
kwa jamii kuhusu umuhimu wake.

Aidha Mhandisi Madoshi amesema
moja ya maeneo yanayotakiwa kuendelea kuwekewa kipaumbele na jamii ni pamoja na
kuhakikisha utunzaji wa mazingira unakuwa jambo endelevu kwani ni moja ya kitu umuhimu
kwa ajili ya Maisha ya kila siku ya viumbe hai.

Ikumbukwe Dkt.
Heladius M. Makene ni mtaalamu wa mazingira na jamii nchini Tanzania,
anayehusishwa na shughuli za usimamizi wa mazingira na maendeleo ya jamii
katika sekta ya miundombinu na madini. Katika
eneo la
jamii na mazingira
, Dkt.Madoshi amekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira,
ikiwa ni pamoja na kampeni ya “
Barabara
na
Mitaro siyo Jalala,” ambayo inalenga
kuhamasisha wananchi kutunza miundombinu ya barabara kwa kuepuka kutupa taka
ovyo
.

Pia Dkt.
Makene pia amehusika katika tafiti kuhusu athari za kijamii na kimazingira za
sekta ya madini nchini Tanzania. Alishiriki katika utafiti uliochapishwa kwenye
jarida la Resources unaoitwa “Calling for Justice in the Goldfields of
Tanzania,” ambapo alishirikiana na watafiti kutoka Clark University. Utafiti
huo uliangazia changamoto zinazowakumba jamii zinazozunguka migodi ya dhahabu,
hususan kuhusu haki za kijamii, mazingira, na ushiriki wa jamii katika maamuzi

Kwa ujumla, na hitimisho ni kwamba pamoja na kuwa mstari wa mbele katika masuala ya
Mazingira bado
Dkt. Heladius Makene anaendelea kuwa ni mmoja wa wataalamu wa mazingira nchini wenye
uzoefu mpana katika masuala ya mazingira na maendeleo ya jamii, na mchango wake
unaonekana katika jitihada za kuhakikisha maendeleo ya miundombinu na sekta ya
madini yanazingatia ustawi wa jamii na uhifadhi wa mazingira.

Mwisho.

 

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.