Hatua ya Marekani ya kuwawekea vikwazo vya usafiri maafisa wakuu wa tume ya uchaguzi pamoja na viongozi wengine nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya DRC imeendelea kuzua hisia mbalimbali.
Serikali ya Marekani ilichukua hatua hiyo mwishoni mwa wiki kwa madai kwamba viongozi hao walijipatia utajiri kwa njia za rushwa.
Msemaji wa Tume huru ya uchaguzi Jean Pierre Kalamba, kupitia barua iliyotiwa saini na tume hiyo amekanusha tuhuma hizo za rushwa na kuongeza kuwa ilifanya kazi nzuri ya kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa njia ya amani.
Hali ambayo ilisaidia marais wawili wa Congo kupokezana madaraka kwa njia ya amani.
Bwana Kalamba ameahidi kutoa ripoti ya maandalizi ya uchaguzi kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka huu.
Kwa upande wake Lambert Mende ambaye alikuwa msemaji wa serikali ya Joseph Kabila amesema vikwazo hivyo havitakuwa na mafanikio yoyote.
”Marekani inasimama na watu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kufuatia historia waliyoweka kwa kufanikisha mchakato wa viongozi kupokezana madaraka kwa amani. Uchaguzi ulionesha ari ya wakongo ya kutaka mabadiliko ya serikali na taasisi zinazowajibika. Hatahivyo, kuna madai kwamba hapakuwa na uwazi katika machakato wa uchaguzi.” ilisema taarifa iliyotolewa na Marekani.
Viongozi waliyowekewa vikwazo ni pamoja na mwenyekiti wa tume ya huru ya uchaguzi ya Congo DRC (CENI), Corneille Nangaa, naibu wake Norbert Basengezi Katintima.
from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2SXi3eI
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







