
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambazo kitaifa zinafanyika leo mjini Moshi
Samia aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana jioni, wakati Rais Magufuli na Waziri Mkuu waliwasili tangu juzi wakitokea mkoani Dodoma.
Rais Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zinazofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani hapa iliyoanza juzi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, Rais Magufuli atazungumza na wafanyakazi wote nchini kupitia sherehe hizo kwenye uwanja huo.
Aidha, inatarajiwa kuwa pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli atatoa maelekezo kuhusu kilio cha vyama vya wafanyakazi ambacho ni pamoja na kukosekana kwa mikataba ya hali bora kazini.
“Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika kilele cha sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) ambazo kwa mwaka huu zinafanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.
Pia nashauri wafanyabiashara watumie fursa hii kufanya biashara zako kwa ukarimu na uaminifu mkubwa ili kuwavutia wageni wanaoingia Moshi na watakaoendelea kuja,” alisema Sadiki
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





