Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, ambaye ameugua homa ya mapafu na mkamba kwa zaidi ya wiki tatu, ameonesha shukrani kwa wahudumu wa afya wanaomhudumia, akiwapongeza kwa huduma yao yenye huruma na upendo.
Kwa Jumapili ya nne mfululizo, Papa hakuhudhuria ibada ya baraka za kila wiki, lakini Vatican ilitoa ujumbe wake wa maandishi, akieleza hisia zake za shukrani kwa madaktari na wahudumu wa afya waliopo katika Hospitali ya Gemelli jijini Roma.
“Nikiwa hapa, ninawaza juu ya watu wengi wanaowahudumia wagonjwa,” amesema Papa Francis, akiwaita wahudumu wa afya kuwa “mwanga mdogo katika usiku wa maumivu.”
Taarifa kutoka Vatican imethibitisha kuwa Papa Francis ameonesha mwitikio mzuri wa matibabu katika siku za hivi karibuni, huku akiendelea kupata nafuu.
Katika ujumbe wake, Papa Francis amesisitiza kuwa huruma na utu wa wahudumu wa afya ni baraka kubwa kwa wagonjwa, akisema, “Tunahitaji huu – muujiza wa wema – ambao wale walio katika dhiki wanauhitaji.”Amehitimisha kwa kueleza kuwa huduma za kitabibu zinapochanganywa na upendo na huruma, huwa faraja kubwa kwa wagonjwa na kuwasaidia kuvumilia changamoto za afya wanazokabiliana nazo.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







