Siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, kudai hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mikutano ya hadhara ni ukorofi na uvunjifu wa sheria, uongozi wa chama hicho cha upinzani umemjibu, ukidai kauli yake hiyo ni ya watu wasiopenda kufikiri.
Wiki iliyopita, Chadema kupitia Katibu Mkuu wake, Dk. Vicent Mashinji, ilitangaza kuwa inatarajia kuanza mikutano ya hadhara baada ya kukamilisha mambo yake ya ndani.
Chama hicho kilieleza kuwa kinatambua kuwapo kwa zuio la serikali kufanya maandamano na mikutano ya siasa nchini, lakini kitaendesha mikutano hiyo kwa kuwa iko kisheria na kwamba CCM wamekuwa wakiifanya bila kuchukuliwa hatua.
Baada ya Chadema kutangaza uamuzi huo huku wakiitaja CCM kukiuka agizo la Rais John Magufuli la Juni 23, 2016, ya kuzuia mikutano ya siasa na maandamano, Polepole alizungumza na gazeti la Nipashe kuhusu kauli hiyo na kudai chama hicho cha upinzani kutangaza kufanya mikutano nchi nzima, ni ukorofi na uvunjifu wa sheria.

Akijibu kauli hiyo ya Polepole jana, Dk. Mashinji, alidai kauli ya Polepole ni ya mtu mvuvi ambaye anapinga kitu bila ya kuwa na hoja.

”Hiyo ni kauli ya watu wavivu ambao hawapendi kuzihangaisha akili zao kupinga hoja zinazotolewa,” Dk. Mashinji alisema, “kufanya mikutano ni uvunjifu wa sheria? Hebu atuambie ni sheria au kanuni ipi anayozungumzia hapo ambayo inakataza mikutano.

”Hawa ndiyo vijana wa CCM ambao wamepewa nafasi bila kuandaliwa, hawajui wazungumze nini. Sisi tutaendelea na programu zetu za mikutano kama tulivyoeleza awali.
“Polisi wetu hawana shida, tunawaandikia barua kuwataarifu kuhusu mikutano yetu, wanakuja wanatulinda, hawana shida na sisi. Sasa huyu Polepole anazungumzia sheria ipi au kuna kanuni ipi inayozuia mikutano?”
from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2V8uReJ
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







