Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema chama chake kimeweka lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 100 kupitia harambee ya kitaifa itakayozinduliwa rasmi kesho saa 11 jioni katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za CCM Makao Makuu, Lumumba mkoani Dar es Salaam, Agosti 11, 2025, Dkt. Nchimbi amesema uamuzi wa kuandaa harambee hiyo umetokana na hamasa kubwa iliyojitokeza kwa wanachama wa CCM kutaka kuchangia kampeni.
“Kwa wakati ule kulitokea hamasa kubwa kwa wanachama wa CCM kutamani kuchangia michango ya kampeni. Kutokana na hamasa hiyo, sisi kama Kamati Kuu tumeamua sasa kuwashirikisha wanachama wetu katika uchangiaji kesho saa 11 jioni katika ukumbi wa Mlimani City,” amesema Dkt. Nchimbi.
Akizungumzia malengo ya kuchangia, amesema “Tunachokusudia kupata kwa kiwango cha kawaida ni Bilioni 100. Wanasiasa kokote walipo wajue hiyo ndiyo target tunayokusudia. Kuhusu vyama vingine, tutafarijika sana vikichangia, kwa sababu haihitaji ushahidi wa kipolisi kujua CCM inatumikia Watanzania na vyama vingine vyote.”
Kuhusu udhibiti wa fedha haramu, Dkt. Nchimbi amesema “Jitihada yetu kubwa sisi kama CCM ni kujiepusha kuwa Serikali, kwa hiyo sisi siyo taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu. Wenye kazi yao wataendelea kutafuta fedha hizo, sisi tutaendelea kufanya kazi ya siasa, kwa maana kitu kinachoharibu nchi ni chama cha siasa kuendelea kufanya kazi za dola.”
Harambee hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






