Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wasanii chini kuiga mambo yenye kuleta manufaa kwa jamii.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akihutubia Wasanii wa Sanaa mbalimbali waliohudhuria Kongamano la Wasanii nchini dhidi ya tatizo la dawa za kulevya.
“Naamini kuwa wasanii hawa ni vioo vya jamii lakini baadhi yao wamekuwa wakitumika kama ‘mapunda’ kusafirisha dawa na wengine kudumbukia kwenye uraibu wa dawa za kulevya” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais aliwaasa wasanii hao kujiepusha na matumizi na biashara ya dawa za kulevya ambapo aliwaambia dawa za kulevya zina madhara mengi kiuchumi, kisiasa, mazingira, kiafya na kijamii, pia hudhoofisha afya za watumiaji na kuathiri uwezo wa kufanya kazi.
Kongamano hilo lililobeba kauli mbiu inayosema Usanii bila kutumia au kubeba Dawa za Kulevya inawezekana, Chukua Hatua.
Makamu wa Rais amepongeza kwa kuanzisha vituo 6 vya huduma ya methadone ambapo jumla ya waathirika 6,300 wametibiwa kwenye vituo hivi.
Makamu wa Rais ameagiza Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuharakisha miongozo hiyo na itakuwa vyema ikiwa kwenye udhibiti wa Dawa za hospitali zenye asili ya kulevya ili zitolewe na Bohari ya Kuu ya Madawa (MSD) badala ya watu binafsi.
Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Rais ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama hususani polisi na maafisa uhamiaji kuhakikisha kuwa bidhaa zinazovuka mipaka yetu zisiwe bidhaa zinazokuja kuharibu Taifa.
Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Walemavu) Mhe. Jenista Mhagama alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amedhamiria kutokomeza dawa za kulevya hapa nchini.
Wakati huohuo, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harisson George Mwakyembe alisema amefurahishwa na nia njema iliyoonyeshwa na wasanii ya vita dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2E991C2
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







