Ahmed Ally: Kwaheri Mohamed Hussein, Tulibaki nae Kwa sababu hizi hapa

Masama BlogMICHEZOKITAIFA9 months ago278 Views

Ahmed Ally: Kwaheri Mohamed Hussein, Tulibaki nae ila Alishaisa Kiwango…..

Anaandika Ahmed AllyTuna kila sababu ya kujipongeza kwa maamuzi sahihi tuliochukua kwa Nahodha wetu kipenzi Mohamed Hussein

Kwanza ifahamike kuwa tunampenda, tunamheshimu na hiyo itabaki milele

Ulikua ni muda sahihi wa Tshaba kuondoka Simba na muda sahihi wa Simba kuachana na TshabaKwenye hili agano sio Simba sio Tshaba ambae amepata hasara kila mmoja amenufaika na maamuzi haya

Kwa sasa wataibuka wengi kulaumu lengo lao kuonesha kuwa Simba tumekosea pili kuwapa faraja waliomchukua na tatu ni kutufinitisha sisi na Tshaba pamoja na mashabiki

Ukweli ni kwamba tumepoteza aliyewahi kuwa mchezaji wetu bora sana

Miaka mitatu nyuma mchezaji wetu mmoja ambae pia alikua Nahodha alimaliza Mkataba, Viongozi wakaona taabu kumuachia kutokana na heshima yake tukamuongezea Mkataba wa miaka miwili

Kilichofuatia miaka yote miwili alikaa Benchi na kama haitoshi zipo nyakati alisumbuliwa na Majeraha na akaacha kucheza na akaenda kufundisha timu ya vijana akiwa bado ana mkataba wa Uchezaji

Hayo yote yalitokea kwa sababu hatukutaka kuupokea ukweli kuwa muda wake uliisha tukabaki nae kwa sababu historia na heshima

Ndugu zangu Wana Simba kwa hili tutembee kifua mbele tumefanya maamuzi kwa kuangalia Simba bora ya keshoWala tusiingie ubaridi kwa kua anaenda upinzani wameshaenda wengi na hakuna maajabu

Muhimu sasa ni kuwahimiza Viongozi wetu kusajili mchezaji mwingine kama Tshabalala au zaidi ya Tshabalala

Na hapo sina shaka na viongozi wetu watafanya hilo kwa sababu maandalizi yalishafanyika muda mrefu

Kila la heri Captain @official_mohamedhussein15 Mungu akusimamie, Sisi tunakupenda sana

Wana Simba tusonge mbele mpaka tuko salama kwa sababu hakuna kinachotokea bahati mbaya!!!

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.