
Kati ya magonjwa yanayoathiri watu wengi sana duniani ni magonjwa ya zinaa. Haya ni magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitendo vya ngono.
Vitendo hivi vya ngono vinaweza kuwa kujamiana, kupiga denda (kissing), vitendo vya ngono kwa kutumia mdomo (oral genital sex), kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) iwe kwa mwanamume na mwanamke au kati ya wanaume wenyewe na hata wale wanaotumia vifaa vya kufanyia ngono (vibrators).
Magonjwa ya zinaa huathiri sana watu walio katika umri wa miaka 15 – 24 lakini hata kwa watu wengine ambao wana umri chini au zaidi ya huu niliotaja pia yanaonekana kwa wingi.
Kuna magonjwa ya zinaa zaidi ya ishirini yanayotambulika duniani, baadhi ya magonjwa ya zinaa ni
- Kisonono (Gonorrhoea – “Gono” kama wengi wanavyopenda kuita kwa kifupi).
- Chlamydia
- Kaswende (Syphillis)
- Human papilloma virus (HPV)
- HIV/AIDS (Ukimwi/Upungufu wa kinga mwilini)
- Hepatitis B, C, A
- Herpes virus
- Trichomoniasis
- Bacteria Vaginosis
- Pubic lice (chawa kwenye nywele za kinena)
- Chancroid
Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika lakini kuna baadhi ambayo hayana tiba ya uhakika kama HPV, Hepatitis B na C, na HIV. Mengine yameanza kuwa sugu kutokana na matumizi ya dawa za antibiotics bila mpangilio, magonjwa hayo ni kama gono (gonorrhoea) na nk.
==>>Leo tutazungumzia ugonjwa wa Chlamydia
Kutokana na ukosefu wa takwimu za nchi nyingi barani Afrika ikiwemo Tanzania, ni vigumu kujua idadi kamili ya maambukizi, ingawa bila shaka ndio ugonjwa wa zinaa utokanao na bakteria unaoongoza kwa maambukizi ukifuatiwa na ugonjwa wa gonorrhea.
- Kujamiana kwa njia ya mdomo, njia ya haja kubwa na kupitia tupu ya mwanamke
- Kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito
- Au kupitia manyoya au vinyesi vya wanyama kama ndege walioambukizwa aina ya Chlamydia inayopatikana kwa ndege kama vile kuku, bata, kasuku nk. Aina hii ya clamydia husababisha aina ya homa ya mapafu ijulikanayo kama psittacosis ambayo huambatana na homa kali yenye nyuzi joto kati ya 39.4 – 41.1 celsius
- Kutokwa na majimaji ya rangi ya njano yenye harufu kali na mbaya sehemu za siri
- Maumivu wakati wa kukojoa (haja ndogo)
- Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa
- Kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi yaani baada ya kumaliza mzunguko wa hedhi na kabla ya kuanza mzunguko mwengine wa hedhi
- Maumivu sehemu ya chini ya tumbo
- Maumivu wakati wa kujamiana
- Kutokwa na damu wakati wa kujamiana
- Kuvimba na maumivu kwenye tezi zilizopo sehemu za siri
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa
- Kutokwa na majimaji kwenye uume yanayoweza kuwa ya rangi nyeupe kama maziwa, kijivu au ya njano
- Sehemu ya tundu la uume huwa jekundu, huvimba na kuwasha
- Maumivu kwenye korodani
- Tezi zilizopo sehemu za siri huvimba na huambatana na maumivu
- Kuwashwa na kutokwa na damu kwenye puru
- Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
- Kutokwa na uchafu kama kamasi kwenye puru
- Kuvimba sehemu za macho
- Macho kuwa mekundu, kuwasha na hata kutokwa na majimaji
- Urethral swab for culture – Majimaji kutoka kwenye uume au uke huchukuliwa kwa kutumia swab maalum ambapo hupelekwa maabara ili kuotesha na kuangalia aina ya uoto wa bakteria
- Urinalysis (urine test) – Vipimo vya mkojo
- Polymerase Chain Reaction (PCR) – Kipimo cha kuangalia vinasaba vya bakteria na hufanyika maabara.
- Macrolide antibiotics
- Quinolones antibiotics
- Polyketides antibiotics
- Kwa wanaume, Chlamydia huathiri korodani na kusababisha mwanamume kukosa uwezo wa kutia mimba mwanamke (infertility) na maambukizi
- Maambukizi kwenye tezi dume (prostatitis)
- Kwa wanawake, husababisha maambukizi kwenye mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi, na mayai ya uzazi hivyo kusababisha ugonjwa aina ya Pelvic inflammatory disease (PID). Pia huongeza asilimia ya mwanamke kupata mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi (Ectopic pregnancy). Mbali na hilo, mwanamke hupata maumivu sugu ya kwenye nyonga, ugonjwa wa mifupa arthritis aina ya Reiters syndrome. Vilevile, Chlamydia huweza kusababisha ugumba kwa mwanamke kama hatapata tiba.
- Kwa wajawazito, Chlamydia husababisha wanawake kujifungua kabla wakati. Mtoto anaweza kuzaliwa na maambukizi kwenye masikio, sehemu za siri, macho na kwenye mapafu (homa ya mapafu). Kama mtoto hatapata tiba ya haraka ya macho basi anaweza kuwa kipofu.
- Njia sahihi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa ni kuacha au kuepuka kufanya ngono au kujamiana.
- Kwa wanawake wajawazito, ni vizuri kuhudhuria kliniki mapema wakati wa ujauzito
- Wale wenye maambukizi wanashauriwa kuchukua tahadhari ya kutowaambukiza wapenzi wao kwa kufanya ngono salama (kutumia mipira), kuepuka kushika macho kwa kutumia mikono na hata ikiwezekana kuwaepuka wapenzi wao ili kuwalinda na maambukizi.
- Kwa wale ambao wapenzi wao wameambukizwa au wameonyesha dalili za ugonjwa huu, wanashauriwa na wao kupata tiba hata kama hawana dalili zozote.
