Allen Christian na Collin Ndanzi (DSJ)
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi kisutu imeuambia upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera kuwa waende wenyewe kwa mkurugenzi wa mashtà ka nchini (DPP) ili kujua hatma ya barua ya mshtakiwa ya makubaliano ya kuomba msamaha na kukiri kosa ( pre- baggening).
Hatua hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo leo Desemba 4, 2019 ilipoitwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kwa ajili ya kutajwa na kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa utetezi wakawasilisha hoja zao.
Mapema wakili wa utetezi Jebra Kambole alidai mahakamani hapo kuwa, Oktoba 11, 2019 waliitaarifu mahakama juu mshtakiwa kuandika barua ya kuomba msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP .
“Ni lini tutakamilisha mchakato wa majadiliano hayo kwani mpaka sasa hakuna chochote ambacho kimefanyika na mtuhumiwa bado yuko gerezani na ni mgonjwa”, ameuliza Kambole
Akijibu hoja hizo wakili wa serikali Easter Martin amekiri kwamba ni kweli maombi yao hayo yapo kwa DPP toka Oktoba 11 hadi leo lakini suala la makubaliano si maamuzi yanayoweza kutolewa mara moja, ni vema waende katika ofisi ya DPP ili wajue kinachoendela.
Hakimu Mtega nae amesema, kufuatia hoja hizo, amewataka upande wa utetezi waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba 18, mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.
Katika mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.
Mwimsamaha na kukiri kosa ( pre- baggening).
Hatua hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo leo Desemba 4,2019 ilipoitwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kwa ajili ya kutajwa na kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa utetezi wakawasilisha hoja zao.
Mapema wakili wa utetezi Jebra Kambole alidai mahakamani hapo kuwa, Oktoba 11,2019 waliitaarifu mahakama juu mshtakiwa kuandika barua ya kuomba msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP .
“Ni lini tutakamilisha mchakato wa majadiliano hayo kwani mpaka sasa hakuna chochote ambacho kimefanyika na mtuhumiwa bado yuko gerezani na ni mgonjwa”, ameuliza Kambole
Akijibu hoja hizo wakili wa serikali Easter Martin amekiri kwamba ni kweli maombi yao hayo yapo kwa DPP toka Oktoba 11 hadi leo lakini suala la makubaliano si maamuzi yanayoweza kutolewa mara moja, ni vema waende katika ofisi ya DPP ili wajue kinachoendela.
Hakimu Mtega nae amesema, kufuatia hoja hizo, amewataka upande wa utetezi waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba 18, mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.
Katika mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2rPBiKu
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








