Na Grace Gurisha
MENEJA Mauzo na Masoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali ya kiteknolojia ya MD Technology, Mohamed Kaddy amesema wameleta kifaa maalumu chenye uwezo wa kudhibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto.
Kaddy aliyasema hayo leo Desemba 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho, ambapo alisema kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana na mmiliki atapata taarifa kupitia simu yake ya mkononi.
Meneja huyo alisema teknolojia hiyo ni rahisi, “Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi,itapatikana tu, lakini pia kama kuna mtu amesimama katika pikipiki yako utajulishwa”,.
“Kifaa hichi maalumu kitafungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja atapata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika simu yake ya mkononi na pia hata akipoteza simu yake anaweza kutumia simu ya mtu mwingine na kupata taarifa kifaa chake kilipo,” alisema
Alisema mfumo huo husaidia kudhibiti udanganyifu wa madereva au marafiki katika matumizi ya umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.
“Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki kupata taarifa kwa haraka pale chombo chake kikitaka kuibiwa au kushikwa na mtu, pia mfumo huo utamsaidia mtu kuzima au kuwasha chombo mahali popote atakapokuwa, kama umeibiwa unauwezo wa kuizima pikipiki yako kabla haijafika mbali,” alisema
Alisema kifaa hicho tayari kimeshaanza kuuzwa kwa bei nafuu, hivyo madereva wajitokeze kwa wingi kununua ili kudhibiti wezi kutokana na wimbi la wizi wa Bodaboda linaloendelea hivi sasa.
Pia, alisema wanafunga vifaa kwenye nyumba kwa mfumo wa kisasa ambapo hata mwizi atakapokwenda kuiba hata gundua kama kuna kifaa cha usalama kimefungwa kwa hiyo itakuwa ni rahisi yeye kukamatwa kwa sababu kifaa kitaonesha kuna mtu ameingia.
Meneja Mauzo na Msoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali yabkiteknolojia ya MD Technology, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kifaa cha kisasa cha kuzuia wizi wa vyombo vya moto.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya MD Technology, Brian Kessy akiwaeleza madereva wa Bodaboda faida ya kifaa hicho ambacho kitawasaidia katika suala nzima la ulinzi wa pikipiki zao
Mtaalamu wa Mifumo kutoka MD Technology, Salum Mntitiwa akionesha jinsi ambavyo kifaa hicho kilivyofungwa na kuunganishwa na simu ya mkononi kinavyoweza kufanya kazi kwa kuliweka gari katika hali ya usalama,
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RUIQGO
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33










