Watu 37 wamefikisha na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital) kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
Tukio hilo limetokea jioni ya leo katika eneo la Mtumba nje kidogo ya Manispaa ya Jiji la Dodoma ambapo walikula chakula hicho wakiwa kwenye msiba wa jirani yao.
Akizungumza hospitalini hapo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi amekiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza tayari ameshaagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi kwenye mabaki ya chakula hicho ili kugundua chanzo chake.
” Mara baada ya kupata taarifa hizi tumefika hapa na Timu ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa kwa hatua ya awali tumesimamia kuhakikisha watu wetu wanapata huduma ya kwanza na kiukweli wagonjwa wote wanaendelea vizuri.
Kati ya hao 37 waliolazwa, wanaume ni 10, wanawake wapo 23 na watoto wakiwa ni wanne, tayari nishatoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo, lakini pia tunafanya uchunguzi wa kitabibu kujua ni sumu ya mtu kuweka au ni sumu ya chakula,” Amesema Mhe Katambi.
Amewataka wananchi kuwa watulivu kwa sasa na kusubiria kupata majibu kutoka kwa Timu inayofanya uchunguzi na kuwataka wale wote ambao wanaona dalili za kuhara na kutapika kufika katika vituo vya afya vilivyopo karibu ili kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Best Magoma amesema hali ya wagonjwa waliofikishwa hospitalini hapo inazidi kuimarika baada ya kuwapatia matibabu na pindi watakaporidhishwa na maendeleo ya afya zao wataruhusiwa kurudi majumbani mwao.
” Tunawashukuru viongozi wetu wa ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya kwa kufika hapa na kutuongezea nguvu, na timu yetu kwa kushirikiana na wenzetu wa Polisi na TBS tumeshaanza uchunguzi wa kubaini nini chanzo cha tatizo hili, nitoe wito kwa wananchi ambao wanaona dalili kama hizi kujitokeza haraka kwenye vituo vya afya na sisi tupo tayari kuwahudumia,” Amesema Dk Magoma.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Q0JMqD
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33











