WAGONJWA waliofikishwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ilifikia 55 ambapo wawili kati yao wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali zao kutengamaa.
Idadi hiyo ya watu walifikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ugonjwa wa kuhara na kutapika kwa kile kinachosadikiwa kula chakula chenye sumu kwenye msiba wa jirani yao eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Akizungumza hospitalini hapo alipoenda kuwajulia hali wagonjwa hao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe DkBinilith Mahenge amewapongeza madaktari na wauguzi wa Hospitali hiyo kwa namna walivyowahudumia wananchi hao kwa haraka na kujitahidi kumaliza tatizo hilo.
Amesema idadi ya waliyofika hospitalini hapo walikua ni 45 lakini baadaye Serikali iliamua kupeleka gari mbili za wagonjwa ambapo wengine 10 walijitokeza na kuchukuliwa baada ya kufanyiwa vipimo.
” Tunawashukuru sana matabibu wetu hakika wamefanya kazi nzuri sana, nimepita wodi zote kukagua hali za wagonjwa ambao wote wamehudumiwa bure wanaendelea vizuri.
Niwaombe wananchi wetu wawe wasafi hasa katika mikusanyiko ya watu, lakini pia niwatake wawe watulivu wakati huu ambao Serikali inafanya uchunguzi wake kubaini nini chanzo cha tatizo hilo, ” Amesema Dk Mahenge.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma amesema utafiti unaendelea kujua chanzo cha ugonjwa huo huku akisema mpaka kufikia jioni idadi kubwa ya wagonjwa watakua wameruhusiwa kurudi majumbani mwao.
” Hali za wagonjwa ni nzuri na wengi wao tutawaruhusu leo kurejea majumbani mwao, jana tulifika kwenye eneo la tukio tukachukua sampo ya Chakula, Maji na Damu kwa ajili ya kufanyia uchunguzi, ” Amesema Dk Magoma.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2S77eoP
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









