Na, Editha Edward -Tabora.
Wakulima wa zao la Tumbaku wilayani Kaliua Mkoani Tabora wametakiwa Kuanzisha Mashamba ya Miti ili kuepusha uharibifu wa mazingira katika vijiji vyao
Ametoa Agizo hilo mkuu wa wilaya hiyo Abel Busalama wakati akizindua kampeni ya upandaji Miti kwa Wakulima wa Tumbaku ndani ya wilaya hiyo
Amesema Miti ni muhimu kwa sababu inachochea uwepo wa mvua unasababisha udongo uwe na rutuba pamoja na kutunza uoto wa asili
Pia amesisitiza ili kunusuru mazingira kutokana uharibifu mkubwa unaochochewa na ukataji Miti kwa ajili ya shughuli za kilimo hivyo Kila mkulima anatakiwa kupanda Miti katika mashamba yake
Busalama pia ameagiza Wakulima wote wanaolima zao hilo kununua mashamba na kupanda Miti ya kutosha ili kuhamasisha makampuni yanayonunua zao hilo kuongeza idadi ya kilo watakazonunua
Aidha amesema wataanzisha msako wa kukagua Kila shamba Kama Miti hiyo itapandwa na endapo kwenye shamba atakapokutwa hajapanda Miti atachukuliwa hatua ikiwemo kuzuiwa kupima hadi atakapopanda Miti
Katika hatua nyingine ameipongeza kampuni inayonunua zao hilo la Tumbaku wilayani humo ya Japan Tobacco International (JTI) kwa kusimamia ipasavyo kampeni ya uanzishaji mashaba ya Miti kwa vyama vya Wakulima wa Tumbaku katika wilaya hiyo
Kwa upande wake Ofisa wa JTI Chrispin Mchafu amesema kampuni hiyo imeanzisha kampeni ya upandaji Miti kwa vyama vyote vya Wakulima wa zao hilo na kuongeza uzalishaji wa Tumbaku.
Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama akipanda mti katika moja ya shamba la mkulima.
Pichani ni baadhi ya wakulima wa Tumbaku wilayani Kaliua Kila mmoja akiwa ameshikilia mche wa mti ili kwenda kupanda mashambani mwao.
Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama akipanda mti katika moja ya shamba la mkulima.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Z6Zg0k
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









