Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk Jamala Taibu kulia akibadilishana hati ya saini na Meneja wa Kanda ya Dare-es-Salaam Bohari kuu ya Dawa MSD Celestine Haule kuhusu mkataba wa makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk Jamala Taibu kulia akitiliana saini na Meneja wa Kanda ya Dare-es-Salaam Bohari kuu ya Dawa MSD Celestine Haule mkataba wa makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda Salome Mallamia akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba kuhusiana na umuhimu wa kupatiwa huduma ya afya na Dawa wananchi katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana saini hati ya makabdihiano ya ununuzi wa madawa kati ya Bohari ya dawa Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuimarisha huduma za afya nchini .
Utiaji saini huo ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Jamala Talib na Meneja wa Kanda ya Dare-es-Salaam Bohari kuu ya Dawa MSD Celestine Haule ambao ulifanyika huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar .
Utiaji saini huo ni wa muda wa miaka mitatu wenye lengo la kutoa huduma kwa kiwango kinachohitajika katika kuboresha usafirishaji wa dawa na ununuzi kutoka kiwandani.
Nae Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa ni busara kutumia huduma za ndani ya Tanzania kwa kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa urahisi.
Aidha alisema kuwa katika utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar ni kuhakisha wananchi wanapatiwa huduma za matibabu bure na kuona mashirikiano yanaimarika katika utoaji wa huduma.
Vilevile alisema idadi imeongezeka ya wagonjwa kwa kuwepo ongezeko la wagonjwa ambao wanahitaji huduma ya tiba na dawa hivyo Serikali imeongeza idadi ya madaktari ili kuweza kutoa huduma.
Hata hivyo alisema kuwa msimamo wa Serikali katika kuimarisha huduma zake imepanga kununua dawa viwandani na sio kwa watu binafsi ili kuona dawa zinakuwa na kiwango kinachohitajika.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Ze3kM7
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







