Na.Khadija seif, Michuzi TV
MLEZI wa kituo cha kulea watoto yatima cha kurasini Bi.Anna amewaomba wazazi kuiona fursa ya kusaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu
Bi.Anna amesema hayo wakati wa sherehe ya kukaribisha sikukuu ya krismas iliyoandaliwa na hoteli ya serena jijini Dar es salaam na kujumuisha watoto yatima kutoka vituo mbalimbali .
“Watoto hawa ni wetu sote jukumu la kuwalea sio la serikali au watu binafsi peke yao bali ni jukumu la Kila mtanzania kwani tukiwaacha tunawatengenezea mazingira hatarishi na kupelekea kujiingiza kwenye vitendo viovu vya ubakaji,ukahaba pamoja wizi na kusababisha nchi kuwa na watu waovu wengi na kurudisha maendeleo ya jamii yetu kuzorota”
Aidha,mama mlezi wa watoto ameeleza changamoto anazopitia katika ukuaji wao hasa wale walemavu ni pamoja na kukosa vifaa vinavyowawezesha kufanya mawasiliano ya usiku kwa viziwi, na baiskeli kwa watoto walemavu wa miguu.
“Kuelekea sikukuu ya Christmas na sikukuu nyingine watu wamekua wakija kituoni na kuwapatia misaada mbalimbali watoto wetu kuonyesha upendo na jinsi gani wanawathamini watoto ,”
Pia amewapongeza uongozi wa hoteli ya serena kwa kuendelea kuonyesha upendo wa dhati kila mwaka na kuwakaribisha watoto na kucheza,kujumuika kwenye chakula pamoja nao.
”watoto wanapokutana na kushiriki michezo inawajengea uwezo wa kujiamini mbele za watu na pia inatupa uhalisia kuwa hata wao wanavipaji vingi na hasa leo tumeona wengi wanajua kuimba na kucheza,”
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35UrIF1
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








