Hatua hiyo leo Januari 20,2020 wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na wakili wa Kabendera, Gebra Kambole kuwasilisha maombi mahakamani hapo.
Mapema wakili Kambole ameiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki Ibada ya Mazishi ya Mama yake mzazi katika Kanisa la Roman Katoliki lilipo Chang’ombe leo mchana akidai kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya Binadamu, suala la faragha.
Amedai, kushindwa kuudhuria maziko ya Mama yake atakuwa ameadhibiwa adhabu kubwa tena kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza hivyo ni vizuri akatoa heshima ya mwisho
Wakili Jebra amedai kuwa ni muhimu kwa Kabendera kushiriki kwa sababu Mama mzazi ni mmoja, akifa anaagwa mara moja.
“Jamhuri haitaathirika kwa lolote kwa sababu mshitakiwa atakuwa chini ya ulinzi na ibada itakuwa mchana kanisani na Temeke sio mbali na gerezani, tunaomba akatoe heshima ya mwisho,” ameomba.
Akijibu home hizo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega anayesikiliza kesi hiyo kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.
“Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba, akiongeza Kudai kuwa, maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na DPP hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.
“Katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka, hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini mahakama isifungwe mikono,” amesema.
Kuhusu mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefika hatua nzuri baina ya mshtakiwa na (DPP).
Kufuatia home hizo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi saa 8:45 mchana huu kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Kabendera ashiriki Ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi ama lah.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35iHjgL
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







