Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
IRAN imekiri kuidungua kimakosa ndege ya abiria ya Ukraine (Boeing 737) na kuua abiria wote 176 waliokuwamo na kueleza kuwa makosa ya kibinadamu yalitokea baada ya ndege hiyo kukatisha katika eneo linalomilikiwa na kikosi cha Mapinduzi cha nchi hiyo na kueleza kuwa maafisa waliofanya kosa hilo watachukuliwa hatua.
Televisheni ya taifa ya Iran imetoa taarifa hiyo leo ambapo awali Iran ilikanusha kutohusika na udunguaji wa ndege hiyo katika Mji kuu Terhan siku ya Jumatano.
Pia taarifa hiyo imefuatiwa na radhi iliyoombwa na Rais wa Iran Hassan Rouhani ambaye ameeleza kuwa Serikali inajutia kitendo hicho kilicholeta madhara makubwa na kuelekeza maombi na sala zake kwa wafiwa na familia zilizoathirika.
Pia Waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Javad Zarif ameomba radhi kwa familia, wafiwa na mataifa yaliyoathirika na tukio hilo na kusema kuwa ndege hiyo ilidunguliwa kwa bahati mbaya baada ya kupitia sehemu nyeti ya jeshi.
Hii inakuja siku chache baada ya Iran kukana madai ya wachunguzi kutoka nje ambao waliinyooshea kidole nchi hiyo kwa kuhusika
na tukio hilo ambalo mara baada ya kutokea Rais wa Marekani Donald Trump alieleza akuwa Iran inahusika na shambulio hilo huku Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akisema kuwa vyombo vya usalama vya Canada vina ushahidi kuwa Iran imeitungua Boeing 737.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/308BTE4
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







