NA MWANDISHI WETU, RUFIJI
WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere Mw 2115 (JNHPP) uliotimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa utekelezaji wake.
Dkt. Kalemani ameridhishwa na hatua mbalimbali ambazo mradi huo unaotekelezwa kwenye mto Rufiji kwenye mpaka wa mikoa ya Pwani na Morogoro umefikia tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi.
Aidha, alitoa maagizo kwa Wakandarasi kuhakikisha Wafanyakazi wao wote wanahamia eneo la mradi, huku akitoa mwezi mmoja kwa wafanyakazi wengine wa mradi wawe wamehamia. “Wafanyakazi wote wakae eneo la mradi, hii itaharakisha mradi kukamilika mapema na haraka”, alisema Dkt. Kalemani.
Pia, alisisitiza kazi zote zinazohusu utoaji huduma zifanywe na Makampuni ya kitanzania ikiwemo Wakandarasi wasaidizi. Mkataba wa ujenzi mradi wa Julius Nyerere ulisainiwa Desemba 12, 2018 Ikulu Jijini Dar ea Salaam ambapo Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi Februari 14, 2019 na kuanza kazi za maandalizi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi sita, ambapo mwezi Juni 2019 alianza rasmi kazi za ujenzi. Mradi wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika 14 Juni 2022
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, (kushoto), akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius NyerereMw 2115 (JNHPP) wa mto Rufiji mkoani Pwani, Mhandisi Steven Manda wakati alipofanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.
Dkt. Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto kwa waziri), wakati wa ziara hiyo leo Januari 12, 2019.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3a5LBf5
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33















