Na Ripota Wetu,Michuzi Globu ya jamii
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kupitia Shamba la Miti SaoHill limekabidhi madawati katika Shule ya Msingi Mbalwe iliyopo katika Kijiji cha Wami Mbalwe Wilayani Mufindi.
Madawati hayo yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. David Willium kwa niaba ya Shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kuchangia shughuli za maendeleo katika vijiji vinavyolizunguka shamba.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William amesema anaipongeza TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill kwa jitihada wanazozionesha kwa kushirikiana na jamii kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani.
“Nawapongeza sana SaoHill kwa kuwa majirani wazuri wa wananchi, mmetuchangia madawati 30 lakini bado tuna mahitaji ya madawati sehemu nyingine endeleeni kutusaidia,” amesema William
Ameongeza kuwa anatoa mwito kwa wadau wengine wilayani kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo na hivyo viongozi katika maeneo husika kuhakikisha wanasimamia vyema maendeleo hayo.
Aidha Kaimu Meneja wa Shamba la Miti SaoHill Daniel Silima amesema ugawaji wa madawati haya 30 ni sehemu tu ya jitihada za kuonyesha ushirikiano katika jamii inayolizunguka shamba.
Silima amesema hiyo ni sehemu ya kurejesha fadhira kwa jamii ambayo inazunguka shamba kwani wamekuwa ni sehemu kubwa katika ulinzi wa misitu katika Wilaya ya hiyo ya Mufindi.
Hadi sasa TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill limetoa madawati zaidi ya 1,000 katika jamii inayolizunguka shamba ikiwa ni pamoja na nje ya Wilaya ya Mufindi.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2u0oGBm
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







