Waziri Masanja Kadogosa afanya ziara ya kushtukiza katika Mizani ya Puge, mkoani Tabora,abaini mifumo ya mawasiliano kutosomana ,Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa, amefanya ziara ya kushtukiza katika Mizani ya Puge, mkoani Tabora, na kubaini changamoto za mifumo ya mawasiliano kutosomana pamoja na kutokuwepo kwa kamera za ulinzi (CCTV).
Kutokana na hali hiyo, Kadogosa amempa Meneja wa Mizani wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Mussa George, muda wa siku saba kuandaa na kumpatia mpango kazi wa kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa mizani nchini.
Waziri Kadogosa ametoa maagizo hayo akiwa njiani kurejea mkoani Dodoma kwa ajili ya kushiriki vikao vya Bunge la 13.
Akisisitiza umuhimu wa kutekeleza maagizo hayo kwa haraka, Kadogosa amesema anataka kuona bajeti ya kufunga kamera za CCTV ikiandaliwa ili hatua za utekelezaji zianze.
“Fanyia kazi suala hili haraka. Nataka nione bajeti ya kuweka kamera za CCTV. Ninavyoamini, haigharimu fedha nyingi kutekeleza jambo hili,” amesema Kadogosa.
Amesema amekuwa akipokea malalamiko na tuhuma za rushwa pamoja na uzembe katika baadhi ya mizani kutoka kwa wadau mbalimbali, wakiwemo wasafirishaji.
Ameeleza kuwa changamoto za mifumo ya ufuatiliaji zinaweza kudhoofisha usimamizi na kufanya iwe vigumu kubaini na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya rushwa na ubadhirifu.
Kwa upande wake, Meneja wa Mizani wa TANROADS, Eng. Mussa George, amemweleza Waziri Kadogosa kuwa wataalamu wa wakala huo kwa sasa wako mkoani Morogoro wakiendelea na maandalizi ya mfumo wa kuunganisha mizani.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 - Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33