..DIAMOND AAANIKA HADHARANI KUWA NA MTOTO…!!SIYO SIRI TENAA

Admin Updates11 years ago6 Views

Nani aliyekuwa anafahamu kuwa Diamond Platnumz ni
baba? Well, hatujawahi kumsikia popote akisema kuwa ana mtoto lakini
staa huyo wa ‘My Number One’ alikuwa mkarimu wa kutosha kuweza kuelezea
‘furaha ya kuwa mzazi’ kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao maarufu wa
Nigeria uitwao Lobatan Africa baada ya kwenda huko wiki kadhaa
zilizopita alikoshirikishwa pia na mastaa wa huko wakiwemo Waje na Dr
Sid.


Kwenye mahojiano hayo, mtandao huo ulimuuliza: What
have you learnt about fatherhood, now that you’re a father (umejifunza
nini kuhusu ubaba kwakuwa sasa wewe ni baba)

Diamond alijibu: Fatherhood is a
great experience, very humbling. You learn a lot about your children
and the kids and the kinds of things they love. For example, my baby
loves this cartoon that has a catchy song, I think Ben10. Hahaha!! (Kuwa
baba ni kitu kikubwa, kinavutia sana. Unajifunza mengi kuhusu watoto
wako na vitu wanavyopenda. Kwa mfano ‘mwanangu’ anapenda katuni hii
yenye wimbo unaogusa, nadhani Ben 10!

Kumbe Diamond ana mtoto tena mkubwa anayeweza kuangalia na
kuelewa katuni? Swali ni kwanini hajawahi kusikika akisema ana mtoto?
Hata hivyo September mwaka jana, moja ya magazeti ya udaku ya kampuni ya
Global Publisher, yaliandika habari ya kuibuka kwa msichana aitwaye
Sasha Juma aliyedai kuwa amezaa na Diamond.


Sasha akiwa na mtoto anayedai ni wa Diamond

Msichana huyo alidai kuwa likutana na Diamond Mlimani
City jijini Dar es Salaam na akampenda kwakuwa anafanana na Wema Sepetu
(kipindi hicho walikuwa wameachana. Gazeti hili lilisema wawili hao
hawakuchukua muda na wakaanza uhusiano uliowafanya wakutane kimwili na
kupelekea msichana huyo kushika ujauzito.

Lilidai asha alimpa taarifa staa huyo ambaye alimuomba asitoe
mimba kwakuwa atamsomesha msichana huyo aliyefukuzwa shuleni na pia
kuahidi kumlea mtoto huyo.


“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu
sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza
na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya
kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” gazeti hilo lilimnukuu
Sasha.

Lilisema lilipomtafuta Diamond kwa simu ambaye kwa sasa yupo
nchini Kenya, alijibu: Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu!
Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”

So kama Diamond ana mtoto, huenda aliamua kumkubali mtoto huyu
na pengine ndiye mtoto huyu anayependa kuangalia katuni ya Ben 10!

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.