MPYAAA:BILIONEA AMPANGISHA MSANII LULU JUMBA LA KIFAHARI….

Admin Updates10 years ago6 Views

Madai mazito ya kushtua mtaani yanasema kwamba staa wa sinema za
Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mambo yake kwa sasa yapo juu ya
mstari baada ya bilionea kutoka jijini Arusha (jina tunalihifadhi kwa
sasa) kudaiwa kujitosa kumlea akianza kwa kumpangishia jumba kubwa la
kifahari.


Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akiwa na begi la fedha.

Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akiwa na begi la fedha.


TWENDENI USHUANI
Habari hizo za mitaani zilidai kwamba bilionea huyo amempangishia Lulu
mjengo huo wa maana uliopo ushuani maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam.


Kimuonekano, nyumba hiyo iliyoshuhudiwa na wanahabari wetu mwanzoni
mwa wiki hii haina tofauti na ile mijengo iliyozoeleka ya mastaa wakubwa
wa Marekani kwa maana ya kujitosheleza kwa kila kitu ndani yake.


Kwanza ni nyumba yenye fensi kubwa na kuingia getini lazima ujieleze
‘vizuri’ na ukiingia huufikii mlango wa nyumba kwani kuna ‘kamwendo’.


Nje ya nyumba hiyo kuna ‘parking’ ya magari madogo zaidi ya kumi huku
chini kukiwa na tarazo na pembeni kuna bustani nzuri iliyopandwa maua
ya kuvutia.“Amehamia hivi karibuni, anaonekana muda wa kutoka na kuingia
tu.


Nyumba anayoishi staa huyo.

Nyumba anayoishi staa huyo.


“Lulu ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya
kupendwa, kwa hiyo siyo mtu wa kukaa uswazi,” alidai mtoa habari wetu
na kuongeza:


“Bidada kaula maana nasikia jamaa ameahidi kumpa matunzo ya nguvu.
“Alianza kwa kumnunulia lile gari la kifahari la Toyota Rav4 New Model
analotembelea Lulu, sasa naona kamuweka pazuri na kweli nyumba inaendana
na hadhi yake.


ADAIWA KUMPA JEURI YA KUWAFUNIKA KAJALA, WEMA
“Nasikia jamaa amempa jeuri ya kuwafunika kabisa Kajala (Masanja) na
Wema (Sepetu) ambao inasemekana wana mkwanja wa kumwagamwaga ovyo.”


LULU LAIVU!
Kupitia Kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV, Lulu alionekana ndani
ya mjengo huo uliojaa mazagazaga ya thamani.Mjengo huo una makabati
makubwa ya nguo na viatu kiasi kwamba mtu unaweza ukahisi umeingia
kwenye duka la nguo (boutique) na viatu kibao.


Akizungumza kwa kujiamini Lulu alisema kuwa anapenda vitu vizuri hasa
linapokuja suala la kupiga pamba ndiyo maana amejaza pamba kali kwenye
makabati.“Kimsingi sipendi shida, napenda kuvaa vizuri, kula vizuri,
kulala pazuri na mambo yote mazurimazuri,” alisema Lulu.


Elizabeth Michael ‘Lulu’,akiwa kwenye pozi.

Elizabeth Michael ‘Lulu’,akiwa kwenye pozi.


BILIONEA GANI?
Ili kupata undani wa mwanaume huyo, gazeti hili lilichimba ambapo kwa
mujibu watu wa karibu na Lulu, jamaa huyo ni mfanyabishara mkubwa wa
madini jijini Arusha.


“Kama mtakumbuka, huyo jamaa aliwahi kuwagombanisha Lulu na Husna
(Maulid) kwani mwanzoni alikuwa mwanaume wa Husna.“Hivi unajua kabla ya
ishu hiyo, Lulu na Husna walikuwa mashosti lakini baadaye wakawa kama
paka na panya kisa tu ni huyo bilionea,” kilidai chanzo hicho.


LULU ASAKWA
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo ya mtaani, gazeti hili lilimsaka Lulu
hadi nyumbani kwake na lilipomkosa lilimtafuta kwa njia ya simu na
alipopatikana alifunguka:


“Kiukweli kabisa nyumba ninayoishi sasa mimi na familia yangu siyo
kwamba nimepangishiwa wala kununuliwa na sijui bilionea au kigogo
yeyote, hayo ni maneno ya watu tu. Unajua watu wanaongea sana, wanadhani
mimi siwezi kujimudu,” alisema Lulu kwa kujiamini.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.