NAMNA YA KUPATA MPENZI (UA LAKO LA MOYO WAKO)…SOMA HAPA KUFAHAMU NJIA..

Admin Updates10 years ago6 Views



Jambo la msingi unalopaswa kujua ni kwamba, unapoamua kumtafuta mpenzi
wa kweli, lazima utakutana na hali ya kukataliwa kwa mara kadhaa, yani
wote mkiwa wakataaji na wakataliwa (yupo utakaye mkataa na yupo
atakayekukataa).

Watu
wengine wanapokumbana na hali hii, hujikuta wakiwa ni wenye hasira,
mawazo, aibu na kukata tamaa ya kuendelea kutongoza.Watu wengine
hutafuta mtu mwingine haraka haraka ili kuziba nafasi ya kukataliwa,
lakini wengine pia hushindwa kujizuia kurudia kuwakatalia watu wawili
watatu, hivyo huamua tu kumkubalia mwanamke au mwanaume anapokuwa
akimtongoza, hivyo kujikuta amedumbukia katika penzi lisilo na afya.

Unapokataliwa na watu kadhaa, usilichukulie swala hilo kuwa ni swala
zito saaana, kwani watu wengine wanaweza kuwa wanaamua tu, kukukatalia
kwa sababu za kijuu juu tu, zisizo na maana yoyote. Kwa mfano uoga, aibu
n.k.Unapaswa kutulia na kutojutia kwa tendo hilo, bali changamoto kama
hizi hukupatia uzoefu uzoefu katika mahusiano yenye afya.

Weka
mambo katika mtazamo, usiweke asilimia kubwa ya muda wako katika
kutengeneza mahusiano, bali jikite katika shughuli zinazokufanya upate
furaha. Kama vile kufanya kazi zako, kuwa mwenye afya, kuwa na mahusiano
mazuri na familia yako pamoja na marafiki. Utakapojikita katika kulinda
furaha yako, maisha yako yatakuwa sawa na utaonekana kuwa na mvuto kwa
watu wengine na hasa pale utakapokutana na mtu Special kwako.

Kumbuka kwamba hisia za mwanzo mara nyingi huwa sio zakuaminika, hasa
unapokuja katika swala la kutongozana katika mitandao mbali mbali ya
Internet, watu huwa hawaweki uhalisia wao mbele, bila kujali mmekutana
wapi, lini, kivipi, chamsingi kabla ya kuwa karibu sana na mtu, nivyema
ukawa naye katika hali mbali mbali kama vile, wakati wa shida na raha.
Kwamfano utampima mtujinsi alivyokuchukulia wakati wa matatizo na wakati
wa raha.

Kuwa mkweli na muwazi, jivunie ulichonacho, usitake
mtu akupende kwa ndoto zako au matarajio kuwa mtu flani baadaye.
Kwamfano unamwambia mpenzi wako kuwa baada ya mwaka moja nitanunua gari,
au nitapata kazi au nitakuwa msanii. Inapaswa kupendwa vile ulivyo kwa
wakati huo.

Kikubwa zaidi, wekeza kwanza katika mahusiano imara
na sio kukimbilia kufanya mapenzi. Japokuwa katika zama hizi za kizazi
cha sasa ni vigumu mtu kuchukua muda wa kumfahamu mtu kwanza. Unapaswa
kuwa na mtu kwa takribani muda kadhaa ili mfahamu kama mnaendana kitabia
au lah!.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.