WASANII NEY WA MITEGO NA JACK WOLPER KUIBUA MAHUSIANO YA KIMAPENZI UPYA

Admin Updates10 years ago4 Views



Na Musa Mateja
BAADA ya kudaiwa kuwa wapenzi na kisha habari hizo kufifia, hatimaye
penzi la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Mbongo
Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, limeibuka upya ambapo safari
hii Nay ameamua kufunguka hadharani.

Kwa mujibu wa chanzo makini,  wawili hao walianzisha uhusiano wao
mwishoni mwa mwaka jana na sasa mapenzi ndiyo yamekolea hadi kufikia
hatua ya Nay wa Mitego  kuanika hisia zake mtandaoni.
“Wamekuwa wakibanjuka kwa siri sana si unajua Nay ana mchumba wake
Siwema, bado hajafanya maamuzi magumu ya kumtosa,” kilisema chanzo
chetu.

Paparazi wetu alifanikiwa kunasa ujumbe wa Nay wa Mitego  kwenye mtandao
wa Instagram ambao ulionyesha wakiitana kwa majina ya wapendanao
kuonesha dhahiri wawili hao ni wapenzi.
Mbali na kuitana huko, Nay alionesha kuwa amemmisi Wolper ambapo muda
mchache baadaye naye alijibu kwa kuwa amemmisi pia  kisha Nay akaifuta
posti hiyo baada ya kuandamwa na maneno ya wapambe.

lipoulizwa Wolper kama kwa sasa ameamua kutulia na Nay wa Mitego na
mipango ya uhusiano wao ipoje,  alikataa kufunguka moja kwa
moja.“Kiukweli Nay ni mshikaji wangu tu, unajua nini? Kwa sasa siko
tayari tena kumwanika bwana au mchumba wangu kama nilivyofanya mwanzo
kwa Dallas, nitakuja kumweka wazi labda mwanaume nitakayezaa naye au
atakayenioa kabisa,” alisema Wolper.

Kwa upande wake Nay alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Wolper na hatua
ya kuunadi uhusiano wao mtandaoni huku ikifahamika kuwa ana mchumba
mwingine, hakutaka kufafanua zaidi ya kujibu:

“Mimi huwa siangalii nani atasema nini wala atafikiria nini, mimi
nilimmisi Wolper wangu, sikuwa na namna zaidi ya kutumia peji yangu kama
nilivyofanya, tena siku hiyo alikuwa hapatikani hewani nikaamua
kumtupia mtandaoni bila hofu kwani ni mtu wangu wa karibu na siogopi
kitu juu yake,” alisema Nay wa Mitego.
GPL

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.