MAHUSIANO/MAPENZI:…LABDA MWANAMKE UNARINGIA UZURI NA SHEPU YAKO, VIPI HII LA FARAGHA?

Admin Updates10 years ago6 Views



Ulimwengu
wa sasa umejaa wanawake wazuri sana, kila unayemuangalia unaona kuna
vitu f’lani Mungu kamjaalia. Unaweza kukutana na msichana ambaye hana
shepu kabisa lakini sura yake peke yake inamfanya awe tishio kwa
wanaume.


Wapo pia wanawake ambao hawana sura ya mvuto lakini Mungu kawajaalia kuwa na maumbile tata yanayowatoa udenda wanaume wengi.
Kimsingi kila mwanamke ni mzuri. 
Unaweza kukutana na msichana ukaona hana sifa za kuwa wako lakini kwa mwingine ikawa tofauti.
 Ndiyo maana hakuna mwanamke anayefikia hatua ya kuwa na mpenzi na akakosa, kila mtu ana sifa za kupendwa.

Lakini
sasa leo nataka nizungumzie wanawake ambao wako kwenye ndoa lakini ni
mambumbumbu wawapo faragha. Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, kuna
wanawake wazuri kwa kila kitu lakini wamekuwa wakishindwa kudumu katika
ndoa zao.

Wengine ni wazuri lakini wanaishia kuchezewa na kuachwa, yani hakuna mwanaume anayetokea kutangaza ndoa.
Unadhani ni kwa nini? Swali hilo tutalipatia jibu hapa.
 Lakini
pia wapo wanawake wazuri sana ambao ukiwaangalia unaweza kusema Mungu
kawapendelea, yaani ni wazuri wa kila kitu, kuanzia tabia, sura mpaka
shepu.

Cha ajabu sasa wanawake hawa unaweza kukuta wanaongoza kwa kusalitiwa na waume zao.
Unadhani
ni kwa nini? Jibu pia utalipata hapahapa leo. Kikubwa ambacho nataka
kukieleza ni kwamba, wapo wanawake ambao wanajisifu kwa uzuri lakini
wanajisahau katika sehemu moja ya msingi sana,

FARAGHA!
Huenda
bado nimekuacha kwa kusema hivyo lakini unachotakiwa kunielewa ni
kwamba, wapo wanawake ambao wamekosa mbinu sahihi za kuwashika waume zao
na wapenzi hasa katika eneo la faragha.


Wao
wamebaki kujisifia kwamba ni wazuri lakini wanashindwa kujiweka vizuri
kwenye eneo hilo muhimu. Kwa wale wasiojua ni kwamba, mapenzi ni kama
sanaa. Mwanamke anatakiwa kuwa mbunifu na mtundu wa hali ya juu ili
kuhakikisha anamfanya mume au mpenzi wake ahisi amepata mtu sahihi. 

Itakuwa
ni jambo la ajabu sana kama utakuwa ni mwanamke lakini uwapo faragha na
mtu wako unakuwa mshamba wa kutupwa. Yaani unakuwa hujui chochote.
Unadhani katika mazingira hayo utaweza kumzuia mwenza wako asishawishike
kutoka nje?

Ninaposema
hivyo nisieleweke vibaya kwa kuwa najua kuna wale ambao wamekuwa mbali
kabisa na mapenzi, yaani walikuwa hawajihusishi kwa namna yoyote na
mambo ya mapenzi mpaka pale walipokuja kuolewa.

Hao
wamefanya jambo jema ambalo linamfurahisha Mungu lakini sasa umeingia
kwenye ndoa, umeweka jitihada gani za kuhakikisha na wewe unakuwa
mtaalam kwenye mambo yetu yaleee?Unadhani utakuwa sahihi kusema mumeo
hawezi kukusaliti wakati wewe mwenyewe ni mbumbumbu wa kutupwa
linapokuja suala la mahaba? Mimi sidhani kama utakuwa sahihi.

Kitu
muhimu kwa mwanamke ni kuhakikisha unakuwa mtundu na mbunifu wa mambo
ambayo ukimfanyia mumeo, utamzubaisha na asishawishike kutoka nje.Ni
kweli wanaume wanatakiwa kuwavumilia wake na wapenzi wao lakini wanawake
nao wasikubali kupitwa na wakati.

Wajue
kwamba ulimwengu wa sasa una changamoto nyingi za kimapenzi. Usaliti
umekuwa ni mwingi kiasi kwamba kila mmoja anatakiwa kujiaminisha kwenye 
kumridhisha mwenza wake kwa kila nyanja.

Tusiwe
watu wa kuyaacha mambo yajiendee tu, tunapokuwa tumeingia kwenye ndoa
au kuwa na wapenzi tunakuwa ni watu wazima wenye akili. Basi tutumie
akili zetu, maarifa na ujanja wetu kujipa elimu ya kutosha juu ya
mapenzi.

Hilo litakufanya ujiamini na wala usiwe na hofu ya kusalitiwa. 
Tunajua wapo wanaosaliti kwa hulka zao tu, yaani hata wafanyiwe nini kutulia ni vigumu. Hao wala wasituumize vichwa!
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.