JAMAA AMUUA MKE WAKE KISHA YEYE KUJINYONGA MBOZI MBEYA..SABABU NI HIZI HAPA

Admin Updates9 years ago6 Views

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.



Na Mwandishi wetu,Mbeya,Jamiimojablog
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi
wa kijiji cha Malolo Ndugu  Chipunguli Mkisi
(30) amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.
 Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba
 15
mwaka huu majira ya saa 7 mchana
 huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia,
wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.

Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni  Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa  panga  kichwani . 

Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo  ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume
kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga
kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.
Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na
majeraha kwenye vidole na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa
na maneno “kuwa ameamua kumuua mke wake
na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na mahusiana ya kimapenzi na
mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa
Miili ya marehemu
imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya vwawa. ambapo kwa mujibu Kamanda Msangi
uchunguzi wa tukio hilo  unaendelea.
Mwisho.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.