Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea nyema na maandalizi ya sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya.Mimi namshukuru Mungu kwa kila jambo ambalo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu na nimuombe tu anijaalie niwe miongoni mwa wale watakaouona mwaka 2015 wakiwa wazima. Mpenzi msomaji wangu, kilio cha wengi walio kwenye uhusiano ni kusalitiwa na wapenzi wao waliotokea kuwaamini sana. Wapo ambao si tu kwamba wanahisi bali wanawafumania kila kukicha waume/wake zao licha ya imani waliyokuwa nayo kuwa hawawezi kusalitiwa.
Imefika wakati baadhi yetu hatutaki hata kufuatilia nyendo za wenza wetu tukijua kwamba kufanya hivyo ni kujitafutia presha za bure. Labda mimi naweza kuwa na uelewa tofauti katika hili la kufuatilia Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea nyema na maandalizi ya sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya.Mimi namshukuru Mungu kwa kila jambo ambalo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu na nimuombe tu anijaalie niwe miongoni mwa wale watakaouona mwaka 2015 wakiwa wazima.
Mpenzi msomaji wangu, kilio cha wengi walio kwenye uhusiano ni kusalitiwa na wapenzi wao waliotokea kuwaamini sana. Wapo ambao si tu kwamba wanahisi bali wanawafumania kila kukicha waume/wake zao licha ya imani waliyokuwa nayo kuwa hawawezi kusalitiwa.
Imefika wakati baadhi yetu hatutaki hata kufuatilia nyendo za wenza wetu tukijua kwamba kufanya hivyo ni kujitafutia presha za bure. Labda mimi naweza kuwa na uelewa tofauti katika hili la kufuatilia nyendo za wapenzi wetu. Ninachojua mimi ni kwamba, ili uwe na amani moyoni mwako juu ya mwenza wako lazima uthibitishe kama kweli anakupenda na ametulia.
Utafanya hivyo kwa kufuatilia nyendo zake bila yeye kujua na katika kufuatilia kwako ndipo utajua kama kweli umempata mwenza sahihi ama laa. Wapo ambao husimamia kwenye ule msemo kwamba, ukimchunguza sana bata humli! Jamani ule ni msemo tu, tunajua kila mmoja ana mapungufu yake ila ni vyema ukayajua ya wako ili ujue namna sahihi ya kuishi naye.
Nalazimika kusema haya kwa kuwa, kasi ya wapenzi kusalitiana imekuwa ikishika kasi kila siku kiasi cha baadhi kuhisi bila kusaliti hawasikii raha. Yaani wanapatilizwa kila kitu na wenza wao lakini bado wanatoka nje.
Unakuta mwanaume ana mke mzuri anayejua mapenzi na kila kitu lakini bado mwanaume huyo haridhiki. Pia wapo wanawake ambao wamebahatika kuwapata wanaume ‘handsome’, wanaojua mapenzi na kujali pia lakini bado tamaa za usaliti wanakuwa nazo. Ukiuliza kipi kigeni wanachofuata huko nje, jibu hakuna.
Watu wa sampuli hii ni vyema kuwabaini kuliko kubaki na ile imani kwamba, anakupenda na hawezi kukusaliti. Una ushahidi gani kama kweli anakupenda na hakusaliti huko anakopita?
Hivi leo ukiambiwa utaje sababu inayokufanya uamini kuwa mwenza wako hachepuki utatoa sababu gani? Hakika huwezi kuwa nayo, sanasana utaishia kusema unamuamini kwa kuwa hujawahi kumfumania wala kuona dalili za kuzungukwa.
Kizuri ni kwamba, ukifuatilia sana utagundua wengi wetu hutuna imani ya asilimia 100 ya kutosalitiwa. Wengi wetu licha ya wenza wetu kuonyesha wametulia, bado hatuwaamini kupitiliza. Hii yote ni kwa sababu akiamua kukusaliti anaweza kufanya hivyo na wewe usijue lolote.
Nilishawahi kufanya uchunguzi huko nyuma kwa kuzungumza na baadhi ya watu kuhusu hili suala la kusalitiwa. Wengi walikiri kujua kwamba wanasalitiwa lakini wenyewe wanadai ni mambo ambayo wakiyafuatilia hawawezi kudumu kwenye ndoa zao.
Ni kweli niliobahatika kuongea nao kwenye hili ni wachache sana lakini maelezo yao yamenifanya niwe na uhakika wa hiki ninachokiandika leo.
Kipi kifanyike?
Kutokana na maelezo yangu hapo juu utakubaliana na mimi kwamba hakuna anayeweza kusimama mbele za watu na kuthibitisha kuwa hasalitiwi. Kikubwa ni wewe na mimi kuwaamini wapenzi wetu.
Lakini pia hakuna ubaya kama utafuatilia na kujua kama kweli uliye naye ametulia na hachepuki. Usibaki kuamini kibubusa kwamba husalitiwi, wakati mwingine fuatilia nyendo zake bila yeye kujua.
Najua kweli ukifanya hivyo unaweza kugundua madudu mengi kwa huyo uliyenaye na ukajikuta unachanganyikiwa lakini ni bora utakuwa umejua yaliyojificha ili uchague mwenyewe kusuka au kunyoa.
Heri ujue kisha kama huwezi kumuacha, uzungumze naye, abadilike kuliko umuache aendelee kufanya ufuska wake gizani kisha wewe ubaki na imani kwamba ametulia na hawezi kukusaliti.
Lakini kama moyo wako unagoma kumfuatilia mpenzi wako na moyo wenyewe unakuhakikishia kwamba mwenza wako katulia, basi baki na imani yako hiyo.Lakini kwa ulimwengu wa sasa kama utakuwa umejihakikishia kwa asilimia 100 kwamba una mpenzi ambaye hajawahi kukusaliti na wala hafikirii, jiweke kwenye kundi la watu waliobahatika na Mungu awabariki sana.nyendo za wapenzi wetu. Ninachojua mimi ni kwamba, ili uwe na amani moyoni mwako juu ya mwenza wako lazima uthibitishe kama kweli anakupenda na ametulia. Utafanya hivyo kwa kufuatilia nyendo zake bila yeye kujua na katika kufuatilia kwako ndipo utajua kama kweli umempata mwenza sahihi ama laa. Wapo ambao husimamia kwenye ule msemo kwamba, ukimchunguza sana bata humli! Jamani ule ni msemo tu, tunajua kila mmoja ana mapungufu yake ila ni vyema ukayajua ya wako ili ujue namna sahihi ya kuishi naye. Nalazimika kusema haya kwa kuwa, kasi ya wapenzi kusalitiana imekuwa ikishika kasi kila siku kiasi cha baadhi kuhisi bila kusaliti hawasikii raha. Yaani wanapatilizwa kila kitu na wenza wao lakini bado wanatoka nje. Unakuta mwanaume ana mke mzuri anayejua mapenzi na kila kitu lakini bado mwanaume huyo haridhiki. Pia wapo wanawake ambao wamebahatika kuwapata wanaume ‘handsome’, wanaojua mapenzi na kujali pia lakini bado tamaa za usaliti wanakuwa nazo. Ukiuliza kipi kigeni wanachofuata huko nje, jibu hakuna. Watu wa sampuli hii ni vyema kuwabaini kuliko kubaki na ile imani kwamba, anakupenda na hawezi kukusaliti. Una ushahidi gani kama kweli anakupenda na hakusaliti huko anakopita? Hivi leo ukiambiwa utaje sababu inayokufanya uamini kuwa mwenza wako hachepuki utatoa sababu gani? Hakika huwezi kuwa nayo, sanasana utaishia kusema unamuamini kwa kuwa hujawahi kumfumania wala kuona dalili za kuzungukwa. Kizuri ni kwamba, ukifuatilia sana utagundua wengi wetu hutuna imani ya asilimia 100 ya kutosalitiwa. Wengi wetu licha ya wenza wetu kuonyesha wametulia, bado hatuwaamini kupitiliza. Hii yote ni kwa sababu akiamua kukusaliti anaweza kufanya hivyo na wewe usijue lolote. Nilishawahi kufanya uchunguzi huko nyuma kwa kuzungumza na baadhi ya watu kuhusu hili suala la kusalitiwa. Wengi walikiri kujua kwamba wanasalitiwa lakini wenyewe wanadai ni mambo ambayo wakiyafuatilia hawawezi kudumu kwenye ndoa zao. Ni kweli niliobahatika kuongea nao kwenye hili ni wachache sana lakini maelezo yao yamenifanya niwe na uhakika wa hiki ninachokiandika leo. Kipi kifanyike? Kutokana na maelezo yangu hapo juu utakubaliana na mimi kwamba hakuna anayeweza kusimama mbele za watu na kuthibitisha kuwa hasalitiwi. Kikubwa ni wewe na mimi kuwaamini wapenzi wetu. Lakini pia hakuna ubaya kama utafuatilia na kujua kama kweli uliye naye ametulia na hachepuki. Usibaki kuamini kibubusa kwamba husalitiwi, wakati mwingine fuatilia nyendo zake bila yeye kujua. Najua kweli ukifanya hivyo unaweza kugundua madudu mengi kwa huyo uliyenaye na ukajikuta unachanganyikiwa lakini ni bora utakuwa umejua yaliyojificha ili uchague mwenyewe kusuka au kunyoa. Heri ujue kisha kama huwezi kumuacha, uzungumze naye, abadilike kuliko umuache aendelee kufanya ufuska wake gizani kisha wewe ubaki na imani kwamba ametulia na hawezi kukusaliti. Lakini kama moyo wako unagoma kumfuatilia mpenzi wako na moyo wenyewe unakuhakikishia kwamba mwenza wako katulia, basi baki na imani yako hiyo.Lakini kwa ulimwengu wa sasa kama utakuwa umejihakikishia kwa asilimia 100 kwamba una mpenzi ambaye hajawahi kukusaliti na wala hafikirii, jiweke kwenye kundi la watu waliobahatika na Mungu awabariki sana.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





