
NIMEKUWA nikipata malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wasomaji wangu wakielezea jinsi wanavyosumbuliwa na wanaume, wengine wakidai wanataka kuwaoa, wengine wakieleza wazi kuwa wanataka kufanya nao mapenzi tu tena kwa ahadi ya malipo manono.
Kimsingi hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunakoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwashika sehemu zao nyeti bila ridhaa yao.
Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao. Tabia hii huwakera sana baadhi ya wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na uhusiano wao.
Hata hivyo, kuwaepuka wanaume wakware wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa wengi wao hawana akili timamu, muda mwingi wao huwaza kufanya ngono tena na kila mtu watakayemuona bila kufikiria madhara wanayoweza kuyapata baadaye.
Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi tu huko mtaani ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana!
Niseme tu kwamba, wanaume siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti mpenzio wako.
Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala kwamba kila mtu anaweza kumchezea.
Lakini mbali na hilo, unajiwekea mazingira ya kuwafanya wanaume wakuheshimu na kugwaya hata kukutamkia maneno ya kijinga.
Vaa kiheshima, acha utani wa kijingajinga na wanaume na hakikisha unakuwa na tabia ambazo zitawafanya wanaume wakware wajue kwamba wewe ni mtu mwenye ndoa yako usiyetaka kuutia doa uhusiano wako.
Hata hivyo, huko mtaani unakopita unaweza kukutana na mwanaume anayejua fika wewe ni mtu ulie kwenye uhusiano wako lakini anakusumbua kila siku huku akikushawishi kwa njia mbalimbali.
Huyu hutakiwi kumchekea na kumpuuzia, una kitu cha ziada unachotakiwa kukifanya. Nasema hivyo kwa kuwa kuna wanaume vinga’nganizi. Unampa maneno makali ili akukome lakini bado anaendelea kukusumbua.
Inapofikia hatua hiyo jaribu kumshirikisha mpenzi wako au mumeo.
Hiyo itasaidia sana kwani mumeo anaweza kuchukua hatua zinazostahili dhidi yake na hatimaye kuweza kupunguza kasi ya usumbufu huo. Kamwe usithubutu kukaa kimya.
Mbaya zaidi ni kwamba unaweza kukuta shemeji yako ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wako ama mwanaume anayemfahamu vilivyo mumeo akakutongoza. Huyu ni hatari sana na wala usisubiri akutongoze mara mbili. Siku ya kwanza tu atakayokutamkia maneno yake ya kipuuzi, kwanza geuka mbogo, mkaripie kwa ukali kisha mpe taarifa mpenzi wako.
Baada ya hapo, mwanaume huyo hutakiwi kumheshimu, mchukukulie kama mjinga mjinga fulani. Nasema hivyo kwa kuwa mwanaume wa dizaini hiyo akikutokea kisha ukawa unamchekea ipo siku anaweza kukulazimisha kufanya naye mapenzi.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






