Fei Toto Apiga Hesabu za Ubingwa Yanga SC

7 years ago105 Views

Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amesema hawajakatishwa tamaa na matokeo
waliyoyapata ya kufungwa na Simba sc na badala yake wataendelea kupambana kuhakikisha
wanafanya vizuri katika michezo inayofuata ya ligi.

Fei Toto alisema Simba walitumia vyema nafasi moja waliyoipata na kufanikiwa kupata ushindi
huo walioupata.

“Hatukati tamaa, tutaendelea kupambana, niwaombe mashabiki waendelee kutusapoti ili
tupate matokeo mazuri,” ameeleza Fei Toto.

Ameendelea kwa kusema, ‘kikubwa tunajipanga kwa ajili ya michezo ijayo ya ligi na kikubwa
tunataka kuona timu ikiendelea kuongoza ligi na mwishoni mwa msimu tuchukue ubingwa’.

Licha ya kipigo kutoka kwa Simba SC hapo Jumamosi, Yanga SC bado inaongoza Ligi Kuu
Soka Tanzania Bara ikiwa imejikusanyia pointi 58 katika michezo 24 ya Ligi waliyocheza hadi sasa.

from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2SLEx1S
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.