

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Daniel Chongolo ametembelea Chuo Cha Ufundi (VETA) Wilaya ya Ileje ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne wilayani hapa.
Sambamba na kuongea na wanafunzi na walimu wa chuo hicho RC Chongolo pia ametoa zawadi ya seti za jezi pamoja na mipira miwili kwa wanafunzi hao kama sehemu ya kuhamasisha michezo na umoja miongoni mwao
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi Happiness Seneda akiongea na wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi VETA wilayani Ileje katika Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa.






