Soma taarifa mpya kuhusu yule refa aliyekataa Goli la Aziz Ki dhidi ya Mamelod Sundowns

1 year ago115 Views

 Refa Aliyekataa Goli la Aziz K Ala Shavu Fainali Ligi ya Mabingwa

Refa Beida Dahane ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika kusimamia teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa (VAR) katika mechi ya kwanza ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Esperance na Al Ahly itakayochezwa Tunis, Tunisia, Mei 18.
Jina la Dahane limekuwa maarufu nchini tangu alipochezesha mechi ya marudiano baina ya Mamelodi Sundowns na Yanga iliyochezwa Pretoria, Afrika Kusini, Aprili 5.
Katika mechi hiyo, Dahane alitoa uamuzi uliozua mjadala baada ya kutoamuru mpira uliopigwa na Stephane Aziz Ki kuwa bao licha ya kuonekana ulivuka mstari na kuingia golini.
Katika mechi hiyo ya kwanza ya fainali, refa wa kati atakuwa ni Mustapha Ghobal kutoka Algeria.
Katika uteuzi huo wa Caf, mechi ya marudiano ambayo imepangwa kuchezwa jijini, Cairo, Mei 25, refa wa kati atakuwa ni Jean Jacques Ndala kutoka DR Congo.

—-

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.