Mtendaji Mkuu TARURA awataka wakandarasi rufiji kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja

1 year ago117 Views

Rufiji, Pwani

Mtendaji Mkuu wa
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff  amewataka Wakandarasi wanaotekeleza Miradi ya
TARURA ya ujenzi wa Barabara na Madaraja katika Mji wa Ikwiriri na Utete
kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi ili kumaliza Mikataba yao kwa wakati.

Hayo yamejiri
tarehe 8.11.2024 wakati wa ziara ya Ufuatiliaji (Monitoring) wa miradi ya
Ujenzi na Matengenezo ya Barabara na Madaraja katika Mkoa huo wakati wa ziara
ya Mtendaji Mkuu wa TARURA.



Mhandisi Seff
akiwa katika Wilaya ya Rufiji alitembelea jumla ya Miradi Mitano (5) ya Ujenzi
wa barabara na Vivuko/Madaraja na Makalavati katika Mji wa Ikwiriri  na Utete.

Akiwa katika Mji
wa Utete Mhandisi Seff amemtaka Mkandarasi Kampuni ya NRST Ltd anayejenga  barabara ya Utete-Kingupira Km.32 kwa kiwango
cha changarawe kwa kutumia Teknolojia Mbadala (Mult-Enzymic Compound) kuongeza
vifaa kwa mujibu wa Mkataba ili kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha kazi
kwa wakati.

Vile vile
Mhandisi Seff ameridhishwa na kasi ya Mkandarasi Kampuni ya RABCO  Construction 
Ltd  anayejenga Kalavati la
Nambunju pamoja na kuchonga barabara ya Nyamwage ambapo utekelezaji wake
umefikia asilimia 80.


Aidha, Mhandisi
Seff amemtaka Mkandarasi Kampuni ya MAC Contractors Co.Ltd  anayejenga Daraja la Mohoro kuongeza kasi ya
utelezaji kwa kuzingatia Msimu wa Mvua unakaribia.

Mhandisi Seff
aliahidi kurudi tena wiki ijayo ili kujionea hatua mbalimbali za Wakandarasi
hao walizofikia.

Mhadisi Seff
yupo ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya
miundombinu ya barabara katika Mikoa ya Pwani, Mtwara na Lindi.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.