Mkurugenzi Mkuu wa Songas, Nigel Whittaker akikabidhi medali na kombe kwa Faudhia Juma Said na Zaina Yassin washindi wa kitengo cha Biolojia kutoka shule ya sekondari ya Mtwara Girls wakati wa maadhimisho ya mashindano ya sayansi yajulikanayo kama Young Scientist Tanzania, yaliyofanyika katika kumbi za JNICC, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Songas imekuwa moja kati ya wadhamini wa mashindano hayo kwa muda wa miaka nane sasa na hii ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha sekta ya elimu.
Kheri Omar Sheha na Ally Yassin kutoka Shule ya Feza Zanzibar wakipiga picha (Selfie) na Mkurugenzi Mkuu wa Songas, Nigel Whittaker mara baada ya kushinda kitengo cha Biologia wakati wa mashindano ya Sayansi yajulikanayo kama Young Scientist Tanzania yaliyofanyika katika kumbi za JNICC jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Songas imekuwa moja kati ya wadhamini wa mashindano hayo kwa muda wa miaka nane sasa na hii ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha sekta ya elimu.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OEwgLz
via




