Na Charles James, Michuzi TV
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi ameagiza Mhandisi wa Wilaya hiyo, Christian Mlay pamoja na mhandisi anaejenga mabweni kwenye Shule ya Sekondari Kongwa kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Polisi.
DC Ndejembi amefikia hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Shule hiyo na kubaini kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za ujenzi katika Shule hiyo kongwe mkoani Dodoma.
DC Ndejembi amesema ameamua kufanya ziara hiyo baada ya kuona ujenzi wa majengo hayo unaenda taratibu tofauti na mkataba walioingia na mkandarasi huku pia akieleza kutoridhishwa na namna majengo hayo yanavyojengwa.
” Lengo lilikua kukagua maendeleo ya ujenzi huu lakini kama mlivyojionea wenyewe hakuna kitu cha maana kilichofanyika, tulitoa maelekezo kwao cha ajabu hawajayafanyia kazi, mkandarasi anajenga kwa kasi ndogo tena kwa kujisikia, ubora wa majengo ni tofauti na makubaliano tuliyoingia nao, mbaya zaidi kuna ufisadi mkubwa kwenye manunuzi ya vifaa vya ujenzi.
” Mhe Rais anafanya kazi kubwa hizi pesa za ujenzi wa Shule hii kongwe imetoka Serikali Kuu, hatuwezi kuruhusu mambo ya hovyo kufanyika, tumepewa nafasi na Mhe Rais lazima tuwatumikie wananchi kwa uadilifu,” amesema DC Ndejembi.
Amesema ujenzi huo unahusisha mabweni mawili, madarasa mawili na bwalo la chakula ambapo kiasi cha Shilingi Milioni 290 lakini mpaka sasa kiasi kilichobaki ni Shilingi Laki moja tu huku mkandarasi akiwa hajamaliza kazi.
Mhe Ndejembi amesema sababu zilizosababisha majengo hayo kutokamilika licha kutengewa fedha nyingi ni kutokana na kutofuata maelekezo ya Serikali ya kutumia Force akaunti ambapo walitangaza tenda hali iliyosababisha ununuzi wa vifaa vya ujenzi kununuliwa kwa bei kubwa tofauti na ilivyo kawaida.
Hivyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza TAKUKURU kufuatilia bei ya Manunuzi
ya Bidhaa hizo za Ujenzi ,milioni 74 zilizobaki kwenye akaunti zisitume mpaka uchunguzi ukamilike na wale wote waliohusika katika ubadhilifu huo wanachukuliwa hatua kwa kumdanganya na kumdharau Rais,Waziri wa TAMISEMI pamoja na yeye.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mjs Deo Ndejembi (kulia) akitoa maelekezo kwa mhandisi wa ujenzi wa bwalo shule ya Sekondari ya Kongwa.
DC Ndejembi akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa madarasa, mabweni katika Shule ya Sekondari Kongwa.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33m8g3b
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








