Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kikosi cha Yanga kimesafiri asubuhi ya kuelekea Nyanda za juu kaskazini Kilimanjaro kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers utakaopigwa nchini Botswana.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Mwakalebela amesema Kikosi chao kimeamua kuweka kambi mkoani Kilimanjaro ili kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa August 23.
Amesema mazingira ya nchini Botswana yanalingana na hali ya hewa ya Kilimanjaro kwahiyo wameonelea timu ikakae huko kwa muda pamoja na kucheza mechi mbili za kirafiki.
Mwakalebela amesema, watacheza mchezo wa kwanza na Polisi Tanzania iliyopanda ligi kuu msimu huu na pia watacheza mechi ya pili na AFC Leopard ya nchini Kenya ambayo ina historia kubwa na klabu yao katika miaka ya 1970 mechi iliyofanikisha kujenga jengo la Mtaa wa Mafia.
“kuelekea kwenye mchezo wa marudiano ya timu ya Township Rollers, kikosi kitaendelea na mazoezi na pia tutacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania (August 16) na AFC Leopards (August 18),”amesema Mwakalebela.
Amesema Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ameuhakikishia uongozi kuwa wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers na watahakikisha wanapata matokeo ugenini na kufuzu raundi ya kwanza.
Katika hatua nyingine Mwakalebela amesema wamefanya mawasiliano na CAF ili waweze kupata leseni za wachezaji wao watatu kabla ya kwenda kwenye mchezo wa marudiano nchini Botswana
Amesema lengo la Yanga ni kuhakikisha wanakwenda Botswana wakiwa na kikosi chao kamili.
Wachezaji waliukosa mchezo wa kwanza ni mlinda mlango Farouk Shikalo, Moustafa Suleiman na David Molinga.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2N4z4zv
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







