NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kikao cha kwanza baina ya timu ya wataalamu wa masuala ya Mazao ya Chakula hapa nchini ikiongozwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na ya wenzao kutoka Kenya zinakutana hapa nchini leo Agosti 17, 2019 ili kujadiliana namna bora ya kufanya biashara ya mazao hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana usiku Agosti 16, 2019 kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), jijini Dar es Salaam, Mhe. Bashe alisema, kikao hicho ni makubaliano baina ya nchi hizo mbili kukutana na kujadili namna gani wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Kenya watafanya biashara ya mazao ya chakula na iwe biashara endelevu.
“Biashara tayari imekwisha anza na wakati tunaendelea mpaka sasa wenzetu wa Kenya wamekwishanunua jumla ya tani 34,000 kupitia kwa wafanyabiashara wetu na biashara hiyo inaendelea.” Alifafanua.
Alisema timu ya wataalamu kutoka Tanzania itaongozwa na watu kutoka Wizara ya Kilimo, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ili wakae chini na wakubaliane utaratibu wa namna gani wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Kenya watafanya biashara ya mazao ya chakula.
“Sisi Wizara ya Kilimo jukumu letu ni kufanya mambo makubwa mawili, kuhamasisha uzalishaji wa mazao na kufungua masoko ya wakulima wetu ili waweze kufanya biashara.” Alifafanua.
Alisema katika kikao hicho wametaka mamlaka za viwango za Kenya na Tanzania zijumuishwe kwenye majadiliano hayo ili wazalishaji wa sembe waliosajiliwa Tanzania waweze kusajiliwa Kenya Bureau of Standards ili bidhaa zao ziweze kwenda katika soko la Kenya bila vikwazo vyovyote.“Tunatengeneza Government Agreement ambayo itaonyesha mpango kazi (frame work) ya namna biashara hii itafanyika, tumeshaiteua Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo ndiyo itakayokuwa kiongozi msimamizi na kiungo wezeshi katika biashara hiyo.” Alibainisha Mhe. Bashe.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (katikati), akiwa kwenye kikao baina ya ujumbe kutoka Kenya na wataalamu kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao MchanganyikoTanzania (CPB) kwenye kituo cha Uewekezaji Nchini (TIC) jijini Dar es Salaam. Timu ya wataalamu kutoka Kenya na ile ya Tanzania zinakutana leo kujadili namna bora ya kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizo mbili kufanya biashara ya mazao ya chakula kwa njia rahisi na rasmi.
Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Valerian Mablangeti (aliyesimama), akizungumza kwenye kikao hicho.
Naibu Waziri Bashe (katikati), na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Valerian Mablangeti, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kilimo, kutoka Wizara ya Kilimo Nchini Kenya, Bw.Badu Katelo, wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe kutoka Kenya.
Naibu Waziri Bashe, akiwa katika picha ya pamoja kati ya wataalamu wa CPB na ujumbe kutoka Kenya
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33yfaCy
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33











